Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:53

Minneapolis yawafukuza kazi polisi 4 kutokana na kifo cha Mmarekani mweusi


Waandamanaji huko Minneapolis ambapo George Floyd, aliyekuwa hana silaha alikandamizwa chini na afisa wa polisi. Baadae Floyd alifariki katika hospitali ,Minneapolis, Minnesota, Mei 26, 2020. REUTERS/Eric Miller
Waandamanaji huko Minneapolis ambapo George Floyd, aliyekuwa hana silaha alikandamizwa chini na afisa wa polisi. Baadae Floyd alifariki katika hospitali ,Minneapolis, Minnesota, Mei 26, 2020. REUTERS/Eric Miller

Minneapolis imewafukuza kazi maafisa wa polisi wanne waliohusika kumweka chini ya ulinzi Jumatatu Mmarekani mweusi aliyefariki baada ya ofisa mmoja kati yao kumkandamiza shingo yake kwa goti.

Mtu aliyekuwa pembeni alichukuwa picha ya video, na kuiweka katika mitandao ya kijamii na kwa haraka iliweza kuonekana nchini kote Marekani.

Meya wa Minneapolis Jacob Frey alituma ujumbe wa tweet akisema kuachishwa kazi kwa maafisa hao wanne ni “uamuzi sahihi.”

“Hakustahili kufa. Tulichokiona ni kitu kiovu. Kiukamilifu na wazi kimevuruga mambo. Maisha ya mtu huyu yanathamani,” meya alisema. “Ninaamini kile nilichokiona na kile nilichokiona kwa kiwango chochote kile ni kitendo cha makosa. Kuwa mtu mweusi Marekani isiwe ni hukumu ya kifo.”

Muathirika huyo ni George Floyd. Polisi wa Minneapolis wanasema anashabihiana na mshukiwa wa kesi ya kughushi na wanasema maafisa walichukuwa hatua hiyo baada ya Floyd kukataa kuwekwa chini ya ulinzi.

Video hiyo inaonyesha afisa mzungu akikandamiza shingo ya Floyd kwa goti lake ambaye tayari alikuwa amefungwa pingu.

“Tafadhali, tafadhali, tafadhali, siwezi kupumua, Tafadhali,” anasikika akisema hayo wakati watu walioko pembeni wakipiga makelele kumtaka polisi aache kuikandamiza shigo yake.

Afisa aliyekuwa anakandamiza shingo ya Floyd akimtaka “atulie,” lakini anaendelea kuweka goti lake juu ya shingo ya Floyd kwa dakika kadhaa baada ya muathirika huyo kuacha kufurukuta. Mmoja wa walioshuhudia tukio hilo amesema alimsikia Floyd akimwita mama yake kabla ya kukata roho.

Polisi wa Minneapolis wanaahidi uchunguzi kamili wakati FBI itaangalia iwapo haki za kiraia za Floyd zilikiukwa.

Mamia ya watu walikusanyika Jumanne jioni eneo ambalo Floyd alikufa kupinga maafa hayo.

Waliandamana kilomita chache hadi eneo la polisi, ambapo walipambana na polisi waliokuwa wamevalia vifaa vya kupambana na fujo.

Waandamanaji waliharibu gari moja la polisi, walivunja madirisha ya jengo lilioko karibu na kuchafua jengo kwa kulipakaza rangi. Polisi walikabiliana na waandamanaji hao kwa kutumia mabomu ya kutoa machozi na aina nyingine ya vizuizi dhidi ya waandamanaji.

XS
SM
MD
LG