Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:42

Mamia ya waombolezaji wahudhuria maziko ya George Floyd mjini Houston


UMimbaji Michael Tolds akimba "My Soul's Been Anchored" wakati wa ibada ya maziko ya George Floyd katika kanisa la The Fountain of Praise church
UMimbaji Michael Tolds akimba "My Soul's Been Anchored" wakati wa ibada ya maziko ya George Floyd katika kanisa la The Fountain of Praise church

Waombolezi walijaa kwenye kanisa la Fountains of Praise, Houston, Texas siku ya Jumanne kumwaga Floyd aliyekua na umri wa miaka 46, ambae kifo chake kilichotokea akiwa anakamatwa na polisi kimezusha maandamano ya kimataifa dhidi ya ukatili wa polisi na ubaguzi wa rangi.

Wanasiasa, wanaharakati wa haki za kiraia na wasani waliungana na familia kutoa sifa za mtu aliyejulikana kama 'Jitu Mpole' kabla ya jeneza lake la rangi ya dhahabu kusafirishwa kwa kuvutwa na farcis weupe hadi kaburini kando ya kaburi la mamake.

Familia na wagon wahudhuria ibada ya maziko ya George Floyd ndani ya kanisa la The Fountain of Praise
Familia na wagon wahudhuria ibada ya maziko ya George Floyd ndani ya kanisa la The Fountain of Praise

"Tunaweza kulia, tunaweza kuomboleza, tutapata faraja na tutakua na matumaini" alisema kasisi mwenza wa kanasa hilo Mia Wright.

Floyd aliuliwa Mei 25 na afisa wa polisi mzungu aliyemuwekea goti kwenye shingo yake kwa karibu dakika tisa akiwa analia "siwezi kupumua, siwezi kupumua", maneno yaliyogeuka kua kilo cha kuwaleta pamoja waandamanaji.

Kifo chake kimeleta muangaza juu ya mvutano wajadi kati ya jamii ya watu weusi na polisi hapa Marekani, na kwengineko duniani pale maelfu na maelfu ya watu walijitokeza kuandamana katika miji mikuu tofauti kulaani kitendo hicho na kupinga ubaguzi wa rangi.

XS
SM
MD
LG