Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 04:49

Afisa polisi wa Atlanta afukuzwa kazi kwa tuhuma za kumuua mtu mweusi


Picha hii iliyotolewa na Idara ya Polisi ya Atlanta inamuonyesha Rayshard Brooks akiongea na Afisa Garrett Rolfe kwenye eneo la kuengesha magari la mgahawa wa Wendy's, Jioni Ijumaa, Juni 12, 2020, mjini Atlanta. (Atlanta Police Department via AP)
Picha hii iliyotolewa na Idara ya Polisi ya Atlanta inamuonyesha Rayshard Brooks akiongea na Afisa Garrett Rolfe kwenye eneo la kuengesha magari la mgahawa wa Wendy's, Jioni Ijumaa, Juni 12, 2020, mjini Atlanta. (Atlanta Police Department via AP)

Afisa wa polisi mjini Atlanta, Georgia, amefukuzwa kazi baada ya video inayomuonyesha anampiga risasi mtu mmoja mweusi na kuuawa, kutolewa na idara ya polisi mapema Jumapili.

Mkuu wa Polisi wa mji wa Atlanta Erika Shields, amejiuzulu baada ya Rayshard Brooks, umri miaka 27, kuuawa Ijumaa usiku, na kusababisha wimbi jipya la maaandamano mjini Altanta baada ya kuwepo maandamano makubwa ya kulaani kifo cha George Floyd akiwa chini ya ulinzi wa polisi huko Minneapolis yaliyokuwa yamepungua kasi.

Afisa aliyefukuzwa kazi ametambulishwa kama Garret Rolfe, aliyekuwa ameajiriwa Oktoba 2013, na yule aliyesitishwa kazi akiwa analipwa ni Devin Brosnan, aliyekuwa ameajiriwa Septemba 2018, kwa mujibu wa tarifa iliyotolewa na msemaji wa polisi Sajenti John Chafee.

Idara ya polisi pia imetoa picha za video za kamera inayovaliwa na maafisa wa polisi na ile iliyofungwa kwenye gari zao.

Zaidi ya dakika 40 zilipita kati ya muda ambao Brosnan alikuwa akigonga mlango wa gari ya Brooks wakati akiwa ameweka gari yake katika njia ya mgahawa wa Wendy na pale risasi ziliporindima; Rolfe aliwasili katika eneo la tukio dakika 16 baadae.

Mlio wa risasi unasikika katika video hiyo kutoka katika kamera iliyokuwa katika gari la Rolfe na kutoka katika kamera zote mbili maafisa hao walizokuwa wamezivaa, lakini hazikuonyeshwa popote katika video nne zilizorikodiwa na kutolewa na polisi.

Kamera zote mbili zilizokuwa zimevaliwa zilianguka wakati wa purukushani hiyo ambapo Rolfe alikuwa anataka kumfunga pingu Brooks baada ya kuongea naye kwa dakika 20, japokuwa Brooks anaonekana akitaka kupigwa miale ya kumdhibiti kwa chombo maalum kijulikanacho kama Taser kabla ya kupigwa risasi.

Waandamanaji Jumamosi usiku waliwasha moto mgahawa wa Wendy’s ambako Brooks aliuawa usiku moja kabla ya tukio hilo na kuzuia njia ya barabara kuu iliyoko karibu.

Moto huo ulizimwa ilipofika saa tano na nusu usiku, lakini picha za video za kituo cha habari cha eneo zilionyesha moto huo tena majira ya saa kumi alfajiri Jumapili. Polisi wa Atlanta wanasema watu 36 wamekamatwa wakiwa katika maandamano majira ya saa sita usiku.

Meya wa Atlanta Keisha Lance Bottoms alitangaza kujiuzulu kwa mkuu wa polisi wakati wa mkutano na waandishi wa habari mchana Jumamosi na kuamrisha mara moja afisa aliyepiga risasi.

XS
SM
MD
LG