Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 11:00

Warepublican bungeni waungana kwa karibu na mgombea urais Trump kuhusu sera za nje


Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump alipokutana na Waziri Mkuu Israeli Benjamin Netanyahu katika jumba lake huko Mar-a-Lago, Julai 26, 2024, in Palm Beach, Florida.
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump alipokutana na Waziri Mkuu Israeli Benjamin Netanyahu katika jumba lake huko Mar-a-Lago, Julai 26, 2024, in Palm Beach, Florida.

Warepublican katika Bunge wanaunga kwa karibu  na mgombea urais Donald Trump katika masuala kadhaa muhimu ya sera ya mambo ya nje ikiwa ni pamoja na uungaji mkono wa Marekani kwa Israel. 

Mwandishi wa VOA Katherine Gypson anaripoti, wabunge bado wana tofauti kubwa kuhusu China, sera ya ushuru na misaada kwa Ukraine ambayo huenda ikakanganya awamu ya pili ya Trump.

Rais wa zamani Donald Trump katika mkutano wake na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu mwezi uliopita…

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anaeleza: “Hakuna rais amefanya kila ambacho mimi nimekifanya kwa Israel na siku zote tulikuwa na uhusiano mzuri sana.”

Trump awali alimkosoa Netanyahu kwa kushindwa katika usalama anadai aliwezesha shambulizi la Hamas la Oktoba 7. Kutotabirika ni ishara ya sera ya mambo ya nje ya Trump wakati alipokuwa madarakani. Mchambuzi mmoja aliiambia VOA, sera ya mambo ya nje ya chama cha Republican mwaka 2024 inaonyesha kuwa.

Chris Tuttle, Baraza la Uhusiano wa Nje anasema: “Kuna mambo mengi maalum – ambayo yanampa fursa ya kuweza kuiweka sera ya mambo ya nje kwa njia ambayo yeye anaiona inafaa kwa wakati huu, badala ya kujifunga katika sera mwanzoni mwa muhula wake.”

Warepublican wenzake Trump wanadai kuwa mtandao wa kijamii wa TikTok unadhibitiwa na serikali ya China na unaweza kutumiwa kupata habari za watumiaji na kushawishi imani za kisiasa.

Seneta Mitt Romney, Mrepublican anasema: “Sitaki chama cha Kikomunisti cha China kupata data binafsi kuhusu raia wetu, wala kuwa na uwezo wa algorithims ambazo huenda zikaleta propaganda kwa umma wa Marekani.”

Seneta Mrepublikan Mitt Romney
Seneta Mrepublikan Mitt Romney

Lakini Trump alibadili msimamo wake mwaka huu wa kuipiga marufuku TikTok.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican alisema: “Tutaiokoa TikTok. Wanataka kuiharibu TikTok. Kwahiyo, watu wote kwenye TikTok, mpigieni kura Trump.”

Trump pia ameikosoa NATO, akidai nchi wanachama hawalipi mgao wao kwa ajili ya ulinzi. Mgombea mwenza, JD Vance, amekuwa mkosoaji mkubwa sana kwa Marekani kupeleka misaada ya fedha kwa Ukraine.

JD Vance, Republican Mgombea Mwenza alisema: “Tusifanye kosa kwa ujasiri wa wanajeshi wa Ukraine walioko huku, ukweli nikwamba wana viongozi mafisadi sana na serikali huko Ulaya na huenda ikawa ni uongozi wenye ufisadi mkubwa kuliko kokote duniani.”

Huo ni upinzani wa moja kwa moja kwa Kiongozi wa Walio Wengi katika Seneti, Mitch McConnell, ambaye alileta hoja kuwa msaada kwa Ukraine ni muhimu katika kutetea demokrasia huko Ulaya.

Senata Mitch McConnell
Senata Mitch McConnell

Seneta Mitch McConnell, Mdemocrat alisema: “Si swali ambalo limesuluhishwa kwamba Marekani itapambana na uchokozi kwa nguvu kubwa au hata kama itawaunga mkono washirika wake kwa asilimia 100.”

Wachambuzi wanasema wito wa Trump wa kuongeza ushuru kama akichaguliwa kwa mara ya pili huenda ukasababisha mzozo na wabunge wa Republican.

Gordon Gray, Chuo Kikuu cha George Washington anasema: “Inaonyesha mabadiliko katika chama cha Republican tangu mwaka 2016 kwasababu kihistoria Warepublican wamekuwa wafanyabiashara huru.”

Trump ameahidi kuanzisha ushuru wa takriban asilimia 60 kwa China na asilimia 10 kwa uagizaji bidhaa kutoka nchi nyingine kama akichaguliwa.

Forum

XS
SM
MD
LG