Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:11

Kamala Harris amtangaza Gavana wa Minnesota Tim Walz kama mgombea mwenza wake


Gavana wa Minnesota Tim Walz akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria mkutano na Rais wa Marekani Joe Biden na magavana wengine wademokrat katika Ikulu ya Marekani Washington, Julai 3, 2024.
Gavana wa Minnesota Tim Walz akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuhudhuria mkutano na Rais wa Marekani Joe Biden na magavana wengine wademokrat katika Ikulu ya Marekani Washington, Julai 3, 2024.

Kamala Harris amemtangaza Gavana wa Minnesota Tim Walz kama mgombea mwenza wake Jumanne, vyombo vya habari vya Marekani vimeripoti, wakati makamu wa rais akijiandaa kukabiliana na Donald Trump wa chama cha Republican katika uchaguzi wa Marekani mwezi Novemba.

Walz analeta mtazamo wa maeneo ya ndani na miji midogo ya Magharibikati katika kampeni ya chama cha Demokratic huku pia akiwa amefanikisha malengo ya sera huria kama vile kuhalalisha bangi na kuongeza ulinzi wa wafanyakazi kwa jumla.

Ziara ya majimbo ambayo yatachukua jukumu muhimu katika kuamua ni nani atashinda uchaguzi wa Novemba inatazamiwa kufuata, huku kampeni ya Harris ikielekea huko Wisconsin, Michigan, Arizona na Nevada.

Trump kwa upamde wake alimteua Seneta JD Vance kama mgombea mwenza wake wakati wa mkutano mkuu wa Chama chake cha Republican mwezi uliopita.

Forum

XS
SM
MD
LG