Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 03:08

Harris ataka mdahalo na Trump ambaye anahoji utambulisho wa rangi


Election 2024
Election 2024

Katika ushindani wa urais, mgombea wa Republican Donald Trump na mgombea mtarajiwa wa Democratic Kamala Harris wote wako katika safari za kampeni, ambapo Trump alihoji utambulisho wa rangi wa Harris na Harris alitoa changamoto kwa Trump wafanye mdahalo.  

Zikiwa zimebakia siku 100 kabla ya siku ya uchaguzi, mwandishi wa VOA Scott Stearns anaangalia hali ya utambulishi wa rangi na wapiga kura wanasema nini kuhusu wagombea.

Mgombea wa Republican Donald Trump aliwaambia wafuasi wake katika jimbo la Pennsylvania kwamba mpinzani wake Mdemocrat ni laghai.

Mgombea Urais wa Republican

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican alisema: “Wakuu wa chama cha mrengo wa kushoto cha Democratic wamemsimika kibaraka wao ambao wanajipigania wenyewe. Kamala Harris hakupata kura. Amewekwa tu, wamiliki na wanaodhibiti ni wafadhili na wale wenye sauti ambao wameitengeneza kampeni yake na ambao wanaiibia serikali yetu na kujitengenezea mabilioni kwa mabilioni ya dola.”

Mapema juzi, Trump alikuwa na mkutano na waandishi wa habari weusi, ambapo alihoji utambulisho wa rangi wa Harris, ambaye mama yake ni Mhindi na baba yake ni mweusi.

Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican alisema: “Siku zote amekuwa ni mtu mwenye asili ya India, na kuhamasisha urithi wa India. Sijui imekuwaje amekuwa mtu mweusi mpaka miaka michache iliyopita wakati ambapo aligeuka na kuwa mtu mweusi. Hivi sasa, anataka kujulikana kama mweusi. Kwahiyo, sijui. Yeye ni Mhindi au Mweusi?”

Utambulisho wa Rangi wa Harris

Harris kwa muda mrefu amekuwa akijitambulisha kama mweusi na Mmarekani mwenye asili ya Asia Kusini. Tangu amekuwa mgombea mtarajiwa wa urais kwa tiketi ya Democrati, amekuwa katika ushindani sawa na Trump katika majimbo saba muhimu ambayo yanaweza kuelemea upande wowote, kwa mujibu wa ukusanyaji maoni uliofanywa na Bloomberg News na Morning Consult, kwa kiasi kikubwa kuhusu nguvu ya uungaji mkono mkubwa wa vijana, wapiga kura Weusi na Wahispania.

Mgombea Urais wa Democratic

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani anasema: “Kwahiyo, kasi katika ushindani huu inabadilika, na kuna dalili kwamba Donald Trump anaihisi hiyo. Pengine mmeshaona.”

Harris aliuambia mkutano wa kampeni Jumanne huko Georgia kwamba Trump anaonekana kuwa na mengi ya kusema kuhusu yeye lakini hataki kushiriki mdahalo mwezi Septemba kama ilivyopangwa.

Harris ataka Mdahalo na Trump

Kamala Harris, Makamu Rais, Marekani alieleza: “Ndiyo. Donald, nina matumaini utakubali kukutana na mimi kwenye jukwaa la mdahalo kwasababu kama usemi unavyosema, kama unacho cha kusema, nieleze usoni mwangu.”

Harris alitarajiwa kumtangaza mgombea mwenza wake katika siku zijazo na kuna mkutano mkuu wa chama huko Chicago ili kumsaidia kuwashawishi wapiga kuwa kwamba yeye ni chaguo bora kuliko Trump.

Shauku ya Mabadiliko ya Chama

Huko North Carolina, mpiga kura Wanda Cherry anasema ana hamu kuhusu mabadiliko ya chama cha Democratic kutoka kwa Rais Joe Biden kwenda na Harris.

Wanda Cherry, Mpiga Kura, North Carolina anasema: “Nimefurahi kwamba rais amegundua kwamba tunahitaji mtu ambaye ni kijana kuiongoza nchi, mtu ambaye mzuri na ana nia ya kuwania uongozi.”

Hoja ya Kujitayarisha kuwa Rais

Mpiga kura wa Georgia, T. Stanley haamini kuwa Harris yuko tayari kuwa rais.

T. Stanley, Mpiga Kura, Georgia anasema: “Kwanza, yeye kuwa mgombea. Ni kama vile, kwa kweli, linanishtua mimi, kwasababu kwanza, hajajitayarisha kuwa rais. Na inaonekana kama sasa ndiyo yuko tayari kuwa rais.”

Mpiga kura wa Georgia, Phil Ownbey, anasema Harris ameleta nguvu mpya katika ushindani wa urais.

Phil Ownbey, Mpiga Kura, Georgia anasema: “Nitampigia kura, nina hamu kubwa ya kufanya hivyo. Kwa jumla nadhani anaweza kuwa mliberali kiasi kwa masuala fulani fulani, lakini ili kulinda demokrasia yetu, kwa hakika nitampigia kura.”

Madai ya Wafuasi wa Trump

Huko California, mpiga kura Marina George anasema uungaji mkono wa Trump ni wenye nguvu za kutosha kumshinda mpinzani wake.

Marina George, Mpiga Kura, California alisema: “Hataka kuja kwa Kamala Harris, mtu yeyote watakayemuweka, hawatashinda. Inakifanya chama cha Democratic kugawanyika zaidi na haraka sana. Kila kitu wanachofanya ni kizuri kwa Warepublican.”

Kitaifa, ukusanyaji maoni uliofanywa na Bloomberg unaonyesha kuwa Harris na Trump kitakwimu wamefungana huku zikiwa zimebaki siku kama 100 kabla ya Siku ya Uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG