Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Septemba 19, 2024 Local time: 02:01

Mdahalo wa 2: Wagombea urais watarajiwa wa Republican walumbana kwa saa mbili


Wagombea watarajiwa wa chama cha Republican wanashiriki katika mdahalo wao wa pili Jumatano usiku huko Simi Valley, California, Marekani.
Wagombea watarajiwa wa chama cha Republican wanashiriki katika mdahalo wao wa pili Jumatano usiku huko Simi Valley, California, Marekani.

Wagombea watarajiwa wa Republican ambao wanawania uteuzi wakugombea urais wa Marekani walilumbana kwa saa mbili katika mdahalo wao wa pili Jumatano usiku.

Huku uchaguzi wa kwanza wa awali ukiwa chini ya miezi minne kufanyika, washiriki wote wako nyuma ya rais wa zamani Donald Trump katika ukusanyaji maoni, lakini wana matumaini ya kuwapata wapiga kura.

Rais wa zamani Donald Trump
Rais wa zamani Donald Trump

“Haya wamekutana tena…..” kwa mdahalo unaofanyika kwenye maktaba ya Ronald Reagan, warepublican saba wanaowania uteuzi wa kugombea urais wanashiriki katika mdahalo ambao ulifanyika huko California.

Ilichukua dakika chache tu kwa kundi hilo kuanzza kulumbana, kila mmoja akiwa na azma ya kuonyesha umahiri wake.

Katika suala la uhamiaji: gavana wa zamani wa New Jersey Chris Christie alisema atapeleka Walinzi wa Kitaifa kuungana na maafisa wa forodha na mpaka kudhibiti mpaka wa Mexico. China imekuwa adui wakati wa mdahalo huo.

Gavana wa zamani wa South Carolina Nikki Haley alisema huenda atapeleka kikosi cha operesheni maalum kuwashambulia wakuu wa biashara ya madawa ya kulevya wa Mexico, na kuacha mahusiano ya kawaida na China mpaka nchi isitisha mtiririko wa dawa aina ya fentanyl.

Nikkey Haley Namazi
Nikkey Haley Namazi

Mwekezaji wa biotech Vivek Ramaswamy, kuhusu vita vya Russia nchini Ukraine, alisema ni kwasababu Putin ni dikteta mbaya haina maana Ukraine ni wazuri na aliendelea kusema China ndiyo adui ya kweli.

Florida ilipiga marufuku raia wa China kununua mali karibu na maeneo ya vituo vya kijeshi na gavana wa Florida Ron DeSantis alisema anaunga mkono marufuku kama hiyo kote nchini Marekani.

Akiwa hakuwepo kwenye mdahalo huo alikuwa mgombea aliye mbele katika kundi la Warepublican, rais wa zamani Donald Trump, ambaye alichagua kukutana na wafanyakazi huko Detroit, Michigan, ambako Chama cha Umoja wa Wafanyakazi wa Magari wako katika mgomo.

Utafiti uliofanywa na ABC News umeonyesha karibu asilimia 60 ya Warepublican wapiga watamchagua rais wa zamani badala ya wapinzani wake, huku DeSantis akiwa katika nafasi ya pili na asilimia 16.

Baadaye, wagombea waliendelea na mdahalo. Gavana wa North Dakota Doug Burgum aliukosoa utawala wa Biden for mabadilishano ya karibuni ya wafungwa na Iran.

Gavana Burgum, Mgombea Urais wa Republican: “Wamepewa wafungwa watano; sisi tumepewa wafungwa watano. Lakini pia wamepewa dola bilioni 6, ambazo wanaweza kuzitumia kusukuma mbele ugaidi wao na hili ni taifa ambalo ni mfadhili mkubwa sana wa ugaidi katika dunia.”

Makamu rais wa zamani Mike Pence, alimzungumzia bosi wake wa zamani.

FILE PHOTO: Republican U.S. presidential candidates participate in first 2024 campaign debate in Milwaukee
FILE PHOTO: Republican U.S. presidential candidates participate in first 2024 campaign debate in Milwaukee

Pence, Mgombea Urais wa Republican: “Hivi sasa tunaona Donald Trump akiondoka kutoka kwenye ajenda ambayo ilifafanua utawala wetu na inaelezea harakati za warepublican kwa muda wa miaka 50 iliyopita, ambapo walisimama kwenye jukwaa la dunia, hivi sasa Donald Trump anazungumza lugha ya kutuliza na kuondoa.”

Wagombea hawa watapumzika katika mdahalo kwa zaidi ya mwezi mmoja. Mdahalo wa watatu wa Republican utafanyika Novemba 8 huko Miami, Florida, chini ya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu.

Ni ripoti ya Mwandishi wa VOA Carolyn Presuttin.

Forum

XS
SM
MD
LG