Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 19:08

Mdahalo wa Warepublikan wanaowania kuteuliwa na chama chao kugombea urais 2024


Warepublikan wanaowania kuteuliwa na chama chao kugombea urais 2024.
Warepublikan wanaowania kuteuliwa na chama chao kugombea urais 2024.

Warepublican saba wanaowania kuteuliwa na chama chao kuwania urais katika uchaguzi wa Marekani mwaka ujao wanatararajiwa kukabiliana Jumatano usiku  katika mdahalo wao wa pili.

Tukio hilo litakalofanyika katika maktaba ya rais Ronald Reagan huko California halitamuhusisha mgombea wa mbele wa Republican rais wa zamani Donald Trump.

Eneo hilo kwa kiasi kikubwa litakuwa sawa na lile la mdahalo wa kwanza uliopita wa Republican uliofanyika huko Wisconsin ambao Trump hakutokea.

Watakaoshiriki ni pamoja na Makamu wa rais wa zamani Mike pence, Gavana wa zamani wa South Carolina Nikki Haley, gavana wa Florida Ron DeSantis na gavana wa North Dakota Doug Durgum. Wengine ni seneta wa South Carolina Tim scott, gavana wa zamani wa New Jersey Chris Christie na mjasiriamali Vivek Ramaswamy.

Mabadiliko pekee itakuwa ni kutokuwepo kwa gavana wa zamani wa Arkansas Asa Hutchinson ambaye ameshindwa kufikia masharti yaliyowekwa na kamati ya taifa ya Republican.

Warepublican watamchagua rasmi mgombea wao mwezi Julai mwakani kabla ya uchaguzi wa rais mwezi Novemba.

Forum

XS
SM
MD
LG