Wagombea hao wanapambana kwa ajili ya kushinda uchaguzi mkuu huko Wisconsin, ni moja ya majimbo yanayoweza kuamua ushindani wa mwaka 2024. Mwandishi wa VOA Scott Stearns anaripoti kuwa kampeni zinafanya kazi kupata uungaji mkono wa wapiga kura weusi huko Wisconsin.
.
Wapiga kura wa Wisconsin walimchagua Donald Trump mwaka 2016 lakini Joe Biden miaka minne baadaye. Na mara zote ushindani ulikuwa wa karibu. Kwa hiyo, Wisconsin huenda ikaenda upande wowote katika uchaguzi ambao wapiga kura waliokaribia kugawanywa kwa usawa wakigawanya maoni ya umma.
Katika ushindani wa karibu, pande zote zinajaribu kupata mafanikio na wapiga kura wapya.
Kwa Warepublican, hiyo ina maana kujaribu kuingia katika eneo la Wademocrat kihistoria wakiwa ni wapiga kura Weusi, Orlando Owens ni mwenyekiti wa kwanza wa Wamarekani Weusi katika kaunti ya Milwaukee anaeleza haya:
“Nani anaunga mkono elimu ya watoto wako hivi sasa? Nani anaunga mkono biashara za watu weusi hivi sasa? Nani anaunga mkono wazo la kulinda mipaka yetu hivi sasa? Nani anaunga mkono haki za bundk=uk hivi sasa, ambapo unaweza kujilind amenyewe?”
Miaka minne iliyopita, Biden alishinda Wisconsin kwa kura chache 21,000 lakini aliibeba Milwaukee akiwa na zaidi ya kura 145,000. Uchambuzi uliofanywa na Chuo Kikuu cha Marquette unasema asilimia 53 ya mura za ushindi kwa Biden zimekuja kutoka katika maeneo yaliyo na watu weusi wengi.
Orlando Owens, Mwenyekiti wa Kamatiya Republican Kaunti ya Milwaukee anaeleza zaidi: “Milwaukee haina haja ya kuwageukia Warepublican; tunachohitaji ni msukumo – ndiyo maana ni muhimu sana. Kama tunaweza kupata nguvu kidogo hapa mjini, nguvu kidogo huko kwenye kaunti, tutashinda jimbo hili. Tutashinda katika jimbo, tutashinda kote nchini.”
Trump aliwaambia wafuasi wake kwamba mashtaka kadhaa ya uhalifu yamemsaidia kupata kura za watu weusi.
Donald Trump, Mgombea Urais wa Republican anaeleza:
“Watu wengi wamesema ndiyo maana watu weusi wananipenda, kwasababy wameumizwa vibaya sana na kubaguliwa na kwa kweli wameniona mimi kama nimebaguliwa. Inashangaza sana.”
Biden hawezi kumudu kupoteza kura za watu weusi huko Wisconsin, na kampeni yake inafahamu hilo, anasema profesa wa sayansi ya siasa Cathy Cohen.
Cathy Cohen wa Chuo Kikuu cha Chicago amesema: “Watu wengi binafsi ambao wanafuatilia uchaguzi watasema kwamba bila ya Milwaukee, Biden kwa urahisi atashindwa Wisconsin. Nadhani kampeni ya Biden inaelewa hilo. Nadhani tutaona uwekezaji mkubwa katika matangazo na jumbe ambazo zinasema toka uende ukapige kura.”
Biden alikuwa Wisconsin mwezi uliopita akitangaza ufadhili mpya kusaidia kusahihisha kile alichokiita “makossa ya kihistoria.”
Rais Joe Biden anasema: “Kwa vizazi vya watu weusi, brown na wamarekani wazawa, wamarekani wenye asili ya Asia, jamii za asili za wa Hawaii hawakujumuishwa kikamilifu katika demokrasia yetu, na uchumi wetu.”
Kwa Milwaukee, Biden anasema ndiyo maana sehemu mpya za watembea kwa miguu na njia za baiskleli, pamoja na za basi na miundombinu ya kisasa: “Haya ni maboresho ya kubadili maisha. Pia yatafanya iwe rahisi kwa jamii za watu weusi upande wa kaskazini na jamii za wa Latino upande wa kusini ili kuwa na fursa za ajira, shule na nafasi za burudani katika mji na maeneo ya katikati.”
Kinyozi wa Wisconsin Antonio Perkins anasema bado hajafanya maamuzi: “Nina maana, sijafanya maamuzi. Inafurahisha, nilimpigia kura Biden ili kumuondoa Trump madarakani katika uchaguzi uliopita na sasa najionea naelemea zaidi kwa Trump, kwasababu mambo ambayo tulidhani yatakwenda vizuri, kwa kweli yamekuwa mabaya. Kwahiyo, ndiyo, kwa hakika sijui niwe upande gani kwa wakati huu.”
Kutokuwa na uhakika miongoni mwa wapiga kura wa Democrat kunafanya tayari uchaguzi wa Wisconsin kuwa wa karibu sana kwa kampeni zote kuelekea siku ya uchaguzi.
Forum