Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 15:18

Mahakama ya Juu Marekani yaidhinisha Trump kuwepo katika karatasi ya kura


Rais wa zamani Marekani, Donald Trump
Rais wa zamani Marekani, Donald Trump

Majaji kwa kauli moja walibatilisha uamuzi wa mahakama ya juu ya Colorado kumuondoa Trump katika karatasi la upigaji kura

Mahakama ya juu nchini Marekani imempa Donald Trump ushindi mkubwa Jumatatu wakati akifanya kampeni kurejea tena kwenye urais ikibatilisha uamuzi wa mahakama ambao ulimuengua kutoka katika kura ya Colorado chini ya kifungu cha katiba kinachohusisha uasi kwa kuchochea na kuunga mkono shambulio la Januari 6 mwaka 2021 kwenye jengo la bunge la Marekani.

Majaji hao kwa kauli moja walibatilisha uamuzi wa mahakama ya juu ya Colorado wa kumuondoa Trump katika kura ya msingi ya chama cha Republican siku ya Jumanne baada ya kugundua kuwa marekebisho ya 14 ya katiba ya Marekani yalimzuia kuendelea kushikilia wadhifa wa umma.

Trump ndiye mgombea anayeongoza katika uteuzi wa chama cha Republican ili kupambana na rais wa chama cha Democratic Joe Biden katika uchaguzi mkuu Marekani wa Novemba 5. Mpinzani wake pekee aliyebaki katika uteuzi wa chama chake ni Gavana wa zamani wa jimbo la South Carolina, Nikki Haley.

Donald Trump pia alizuiwa kuwepo katika karatasi zaa kura katika majimbo ya Maine na Illinois kwa kuzingatia marekebisho ya 14 lakini maamuzi hayo yaliwekwa wakati wakisubiri uamuzi wa Mahakama ya Juu katika kesi ya Colorado.

Forum

XS
SM
MD
LG