Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:28

Michigan inapiga kura kumpata mgombea urais kwa Democrat na Republican


Jimbo la Michigan linapiga kura kumpata mgombea urais Marekani kwa Democrat na Republican
Jimbo la Michigan linapiga kura kumpata mgombea urais Marekani kwa Democrat na Republican

Kiwango cha ushindi kitaangaliwa kwa karibu kama ishara za kuungwa mkono kwa wagombea wawili katika jimbo hilo muhimu

Wapiga kura katika jimbo la Michigan nchini Marekani wanapiga kura leo Jumanne katika uchaguzi wa awali wa kumpata mgombea urais wa chama cha Democratic na Republican huku rais Joe Biden na rais wa zamani Donald Trump wakitarajiwa kushinda.

Kiwango cha ushindi huo kitaangaliwa kwa karibu kama ishara za kuungwa mkono kwa wagombea hao wawili katika jimbo hilo muhimu, ambao wanatazamiwa kurejesha mtazamo wa ushindani waliokuwa nao katika uchaguzi wa urais wa mwaka 2020 ambapo Biden alishinda.

Michigan ni makazi ya mkusanyiko mkubwa wa Wamarekani wenye asili ya Kiarabu, na kuna upinzani dhidi ya utawala wa Biden kuunga mkono vita vya Israel huko Gaza umesababisha baadhi ya Wa-Democrat kuwataka wapiga kura kutoegemea kokote kwa upigaji kura wa leo Jumanne badala ya kupiga kura kwa Biden.

Trump ameshinda kila jimbo hadi sasa katika kinyang'anyiro cha uteuzi wa chama cha Republican, na kura za maoni katika jimbo la Michigan zilimuonyesha akiwa anaongoza kwa alama za juu katika jimbo hilo.

Forum

XS
SM
MD
LG