Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 14:41

Trump na Biden wafanya kampeni majimbo ambayo matokeo yanaweza kuchukua muelekeo wowote


Rais Joe Biden (kushoto) na Rais wa zamani Donald Trump
Rais Joe Biden (kushoto) na Rais wa zamani Donald Trump

Wakati wapiga kura wa Marekani wanajitayarisha kwa duru nyingine ya chaguzi za awali siku ya Jumanne, Rais wa Marekani, Joe Biden na mpinzani wake wa kisiasa Mrepublican Donald Trump walisafiri mwishoni mwa wiki kwenda  kwenye majimbo ambayo matokeo yanaweza kwenda upande wowote.

Wawili hao walikuwa katika jimbo la Georgia kufanya mikutano ya kampeni.

Mwandishi wa VOA Veronica Balderas Iglesias ametayarisha hoja kuu walizotoa kila mgombea , ambao wanakaribia zaidi kuliko ilivyokuwa kupata uteuzi wa vyama vyao kwa kinyang’anyiro cha urais 2024.

Uhuru wa Marekani utakuwa katika karatasi ya kura mwezi Novemba, alisisitia Rais Joe Biden wakati wa tukio la kampeni huko Atlanta, Georgia. Kabla ya uchaguzi wa awali wa jimbo hilo siku ya Jumanne – aliwakumbusha wapiga kura kuhusu rekodi ya hasimu wake wa Republican, rais wa zamano Donald Trump, kuhusu haki ya utoaji mimba.

Rais Joe Biden alisema: “Aliingia madarakani akiwa na azma ya kuona kuwa sheria ya Roe vs Wade inabadilishwa. Kwa kweli, anajigamba kwa hilo. Ndiyo, alipata alichokitamani na majimbo yanapitisha marufuku ambayo inawafanya madaktari ni wahalifu, wale waliobakwa na waathirika kuingiliwa na ndugu zao kuondoka katika majimbo yao ili kupata msaada.”

Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba ya Hali ya Kitaifa mjini Washington katika Bunge la Marekani.
Rais wa Marekani Joe Biden akitoa hotuba ya Hali ya Kitaifa mjini Washington katika Bunge la Marekani.

Lakini Georgia, Biden alidai, inaweza kusaidia kukinga haki za uzazi kwa wanawake.

Rais Biden anasema: “Nileteeni Bunge ambalo litaunga mkono haki ya kuchagua na nawaahidi, nitairejesha tena Roe vs Wade kama sheria ya nchi.”

Trump pia alifanya kampeni Jumamosi lakini kaskazini magharibi mwa Georgia ambako aliikosoa vikali hotuba ya karibu ya Biden kuhusu Hali ya Kitaifa.

Trump, Mgombea Urais wa Republican anasema: “Ama uwe Mrepublican, au Huru au Mdemocrat aliyekata tamaa, ambapo wako wengi hao. Nyote mnachotakiwa kufanya ni kuangalia jinsi Hali ya Kitaifa ilivyo. Joe Biden asiwe anapiga kelele kwa kukasirika kwa Marekani, Marekani inatakiwa imepigie za kukasirika Joe Biden.”

Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Rais wa zamani pia alikosoa sera za uhamiaji za Biden na kuelezea mauaji ya……….

Muuguzi mwanafunzi Laken Riley hapo Februari 22. Alidai alifariki katika mikono ya mhamiaji wa Venezuela ambaye aliingia Marekani kinyume cha sheria.

Trump alisema: “Alikuwa mhamiaji haramu na hakutakiwa kuwa katika nchi yetu na asingekuwa katika enzi ya sera ya Trump. Biden alitekeleza sera rasmi ambayo wahamiaji haramu, ambao wanaingia Marekani, wanapewa msamaha wa kutofukuzwa nchini.”

Biden, ambaye alitumia neno “haramu” wakati wa hotuba yake ya Hali ya Kitaifa alizugumzia mauaji ya Riley, baadaye aliomba msamaha na Jumamosi alitetea rekodi yake ya uhamiaji.

Rais Biden alisema: “Nilianzisha mpango wa kina, kurekebisha mfumo wetu wa uhamiaji, kulinda mipaka yetu, kufungua njia kwa uraia kwa wale wenye ndoto hiyo na familia zao, wafanyakazi wa mashambani, wafanyakazi muhimu ambao walitusaidia kupitia kipindi cha janga na wao ni sehemu ya muundo wa jamii yetu.”

Baadhi ya matamshi ambayo wagombea wote wawili wa urais watarajiwa walikuwa wamefanana………..

ni dhana ya uharaka kwa wapiga kura kufika kwenye vituo vya kupigia kura na kuvisaidia vyama vyao kuteua wagombea urais.

Wanachama wa Proud Boys kiungana na wafuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano wa hadhara huko Washington, DC, Novemba 14, 2020. Picha na Andrew CABALLERO-REYNOLDS / AFP.
Wanachama wa Proud Boys kiungana na wafuasi wa Rais wa Marekani Donald Trump wakati wa mkutano wa hadhara huko Washington, DC, Novemba 14, 2020. Picha na Andrew CABALLERO-REYNOLDS / AFP.

Trump alisema kuwa: “Nawaomba mjiunge nasi katika jitihada nzuri ya kuiokoa nchi yetu, kuiokoa nchi yetu.. Pamoja, tutabadili ukurasa huo moja kwa moja kwa jinamizi baya la urais wa Biden.”

Rais Biden anaeleza: “Ni ushindani kati ya majeshi yanayoshinda kwenye mapambano kwa ajili ya taifa hili, kati ya wale ambao wanataka kuivuta nyuma Marekani na wale ambao wanataka kuipeleka Marekani mbele.”

Hawaii, Mississippi, Washington na Georgia watakuwa na uchaguzi wa awali kesho Jumanne. Kuwapata wajumbe waote wanaotakiwa au idadi fulani tu kati yao, huenda wakawa ndiyo watatoa mwelekeo wa atakayeshinda utuezi wa urais kwa mgombea yoyote.

Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali

Forum

XS
SM
MD
LG