Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Januari 21, 2025 Local time: 15:23

Hotuba ya Biden kugusia uchumi, haki za uzazi, uhamiaji na vita


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Rais wa Marekani, Joe Biden atatoa hotuba ya Hali ya Kitaifa leo Alhmisi, ambapo anatarajiwa kuzungumzia  jinsi alivyoshughulikia uchumi, haki za uzazi, uhamiaji, na vita vya Ukraine na Gaza.

Lakini kiongozi huyu mwenye umri wa miaka 81 pia atatumia fursa kuonyesha kuwa ana afya nzuri kimwili na kiakili kwa ajili ya kuwania awamu ya tatu.

Uchaguzi wa mwaka hotuba ya Hali ya Kitaifa inampa Rais Joe Biden fursa ya saa kwa ajili ya azma yake ya kutaka kuchaguliwa tena, akijigamba kwa yake katika masuala ya yanayowahusu wapiga kura, kama uchumi, uhamiaji, haki ya uzazi, na misaada kwa Ukraine na Israel….

…na kuelezea yote hayo, na kutoa njia mbadala kama atashindwa.

Ni suala zito kwa rais yeyote – lakini Biden pia anakabiliwa na upinzani juu ya jambo ambalo hawezi kulibadili.

Chris Jackson, Ipsos: “Umma wa Wamarekani bado una wasi wasi kuhusu umri wa Biden na hilo, nadhani, ni changamoto kuu atakayokabiliana nayo wakati akielezea azma yake ya kutaka kuchaguliwa tena.”

White House imeiambia VOA kuwa rais atalenga kwenye masuala kadhaa.

John Kirby, Msemaji wa Usalama wa Taifa, White House alisema: “Anatazamia kwa hamu kubwa kutumia fursa ya kuzungumza na watu wa Marekani, Bunge na kuzungumza kwa uwazi, na dunia kuhusu mambo mengi makubwa ambayo ameyakamilisha katika miaka hii mitatu na nusu kama rais wa Marekani: kuanzia uchumi mpaka elimu mpaka huduma za afya, na ajira. Pamoja na kuwa kwenye jukwaa la dunia na kurejesha uongozi wa Marekani kwenye uwanja wa dunia.”

Wachambuzi wa masuala ya urais wanasema maneno ya Biden yatajikita sana kwenye sera – lakini hamasa itakuja kutoka katika hotuba yake na jinsi atakavyowaeleza watazamaji.

Jeremi Suri, Chuo Kikuu cha Texas alisema: “Nadhani anafurahi kuwa ndani ya Bunge na kujichanganya na wajumbe wa Congress. Kitakachoangaziwa sana katika Hotuba ya Hali ya Kitaifa itakywa ni wakati pale Warepublican watakapopata fursa ya kuonyesha kutoridhia wakati wa hotuba yake – na hata kumbeza – na yeye kujibu kwa uchangamfu, kejeli na kwa ufanisi mkubwa.”

Wachambuzi wa sera za mambo ya nje wanatarajia Biden ataangazia mzozo wa huko Gaza, na kuelezea kwamba amewakaribisha wanafamilia wa Wamarekani ambao wamechukuliwa mateka na Hamas kuhudhuria hotuba yake.

Merissa Khurma, Wilson Center alisema: “Hotuba zilizopita za Hali ya Kitaifa zilikuwa na mwelekeo kidogo wa masuala ya ndani ya nchi. Kwa kweli, kuna masuala ya ndani kwa hali ya sera ya mambo ya nje, hasa kutokana na mzozo wa Mashariki ya Kati. Lakini hili kwa hakika litachukua lengo kubwa la Rais Biden, kwasababu hilo ndiyo liko katika vichwa vya watu pia.”

Wakusanya maoni wanasema mtu mwingineyuko katika vichwa vya wapiga kura pia.

Chris Jackson, Ipsos anaeleza: “Kwa Biden, kitu muhimu ni kuonyesha kuwa anaweza kushinda tena katika uchaguzi dhidi ya Trump. Kwa kweli jambo muhimu atalazimika kuonyesha, hata zaidi kuliko hivyo, ‘je anafanya vizuri katika kazi yake kuhusu uchumi au uhamiaji au masuala yoyote mengine?”

Biden anapata fursa ya kujibu hilo leo usiku.

Ripoti ya Mwandishi wa VOA Anita Powell.

Forum

XS
SM
MD
LG