Rais wa Marekani Joe Biden anawakaribisha viongozi wa bunge leo Jumanne kwa mazungumzo huko White House huku kukiwa na shinikizo la kupata mabilioni ya dola ya msaada kwa Ukraine na kuepuka kufungwa kwa serikali kuu ya Marekani.
Kiongozi wa walio wengi katika Baraza la Seneti Chuck Schumer, Kiongozi wa walio wachache katika Baraza la Seneti Mitch McConnell, Spika wa Baraza la Wawakilishi Mike Johnson na Kiongozi wa walio Wachache katika Baraza la Wawakilishi Hakeem Jeffries wanatarajiwa kushiriki katika majadiliano hayo.
Baraza la Seneti linaloongozwa na Wademocrat lilipitisha mswaada wa usalama wa dola bilioni 95 mapema mwezi huu ambao unajumuisha dola bilioni 61 kwa Ukraine, dola bilioni 14 kwa Israel, takribani dola bilioni 5 kuwasaidia washirika katika Indo-Pacific, ikiwa ni pamoja na Taiwan, na msaada mwingine.
Johnson ameahidi kutouikisha mswaada huo kwenye Baraza la Wawakilishi kwa ajili ya kupigiwa kura, akisema watu wa Marekani wanawataka wabunge kushughulikia matatizo ya ndani, ikiwa ni pamoja na usalama wa mpaka, badala ya kutuma msaada nje ya nchi.
Forum