Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 23:35

Wanaharakati wanawake wapewa tunzo ya ujasiri White House


Mke wa rais Jill Biden na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakikabidhi tunzo kwa Benafsha Yaqoob wa Afghanistan Machi 4, 2024. Picha na REUTERS/Elizabeth Frantz
Mke wa rais Jill Biden na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani wakikabidhi tunzo kwa Benafsha Yaqoob wa Afghanistan Machi 4, 2024. Picha na REUTERS/Elizabeth Frantz

Darzeni ya wanaharakati wanawake kutoka nchi tofauti walipewa tuzo za International Women of Courage kwa harakati zao katika kutetea haki za binadamu na wanawake.

Sherehe hizo zilizofanyika White House mapema wiki hii, mke wa rais wa Marekani Jill Biden na Waziri wa Mambo ya Nje, Antony Blinken wakiwa ni wenyeji wa tunzo hizo.

Alizungumza katika sherehe hizo, kuhusu ushuja wa wanawake hao, waziri Blinken alisema “Walikuwa wanatetea wafanyakazi wa majumbani huko Bangladesh na watu wenye ulemavu nchini Afghanistan.”

Na kuongeza kuwa “walifichua ufisadi uliokuwepo nchini Uganda, walipambana na manyanyaso ya ngono nchini Japan. Walisimama kidete kwa ajili ya watoto katika maeneo yenye vita, ubakaji wakati wa vita huko Bosnia na Herzegovina, mapambano ya demokrasia huko Belarus."

Naye Mke wa rais Jill Biden alisema kuinua sauti za wanawake jasiri, kama zile za washindi wa mwaka huu, ni umuhimu wa kipekee,

“Vitendo vyenu vya kijasiri vinaweza kuchochea wengine kufanya mambo yao makubwa na madogo. Ni wimbo unaovuma wa siku za usoni kupitia sisi, pia tunaweza kutafuta haki, kuwa watetezi wa uhuru,” alisema Bi. Biden.

Miongoni mwa washindi hao alikua mwanaharakati wa Iran, Fariba Balouch.

Balouch alionekana katika dokumentari ya VOA. Yeye ni kutoka kabila lililotengwa na Baluchi na alionyesha mwanga kuhusu mzozo wa haki za binadamu katika majimbo ya Sistan na Baluchistan licha ya kukabiliwa na manyanyaso.

Mke wa rais Jill Biden, mwenyeji wa tunzo hizi zinazofanyika kila mwaka
Mke wa rais Jill Biden, mwenyeji wa tunzo hizi zinazofanyika kila mwaka

Mshindi wa Gambia Fatou Baldeh alizungumza kuhusu mapambano yake kumaliza ukeketaji dhidi ya wanawake.

“Kutokomeza FGM mwaka 2030 ndiyo lengo mahsusi la ulimwengu la Umoja wa Mataifa la Maendeleo Endelevu, lakini bado mwaka 2024 pekee, kuna takriban wasichana milioni 4.4 walio katika hatari ya ukeketaji kote ulimwenguni,”alisema Baldeh.

Ni wanawake 11 walioweza kuja Washington kupokea tuzo binafsi, kwani serikali ya Cuba ilimzuia mpinzani wa serikali Martha Beatriz Roque Cabello kuondoka kutoka kisiwa hicho kuja kupokea tuzo yake.

Kazi za wanawake tisa kutoka Nicaragua, zilikuwa sehemu ya kundi la wafungwa wa kisiasa walioachiliwa mwaka jana, na pia walitambuliwa na mkurugenzi wa Mkakati wa Kisiasa na Uhamasishaji wa White House, Emmy Ruiz. Wanawake hao hawakuwepo kwenye sherehe hizo.

“Wote wamepigana bila ya kuchoka na kujiweka katika hatari binafsi dhidi ya ufisadi, ukandamizaji, ubaguzi, unyanyasaji na heshima,” alisema Emmy.

Wakati wakiwa Marekani, washindi wa tuzo siyo tu walishiriki katika mikutnao ya ngazi ya juu ya sera na kuzungumza hadharani katika matukio mbali mbali, lakini pia walisafiri kwenda Los Angeles kukutana na kufanya kazi na wenzao wa Marekani

Forum

XS
SM
MD
LG