Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 17:51

Wanawake wajasiri duniani watuzwa na serikali ya Marekani


Hafla ya tuzo za wanawake wajasiri mwaka 2024.
Hafla ya tuzo za wanawake wajasiri mwaka 2024.

Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani ilipokeza Tuzo ya Kimataifa ya Wanawake wenye Ujasiri, katika sherehe zilizofanyika Jumatatu katika Ikulu hapa mjini Washington DC.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken na mke wa Rais, Jill Biden, walikuwa wenyeji wa hafla hiyo, ambapo tuzo mwaka huu, zilipewa wanawake kutoka Uganda, Afghanistan, Bangladesh, Belarus, Bosnia na Herzegovina, Myanmar, Cuba, Ecuador, Gambia, Iran, Japan, Morocco na Nicaragua.

Blinken alisema wakati wa hotuba yake: "Wanawake na wasichana wanadhihirisha ujasiri kama huo hata katika maeneo yanayotikiswa na mizozo, na kutokuwa na usalama, huku wakiumizwa kwa kiwango kikubwa na vurugu hizo."

Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 2007 na hutolea kwa wanawake "ambao wameonyesha ujasiri, nguvu, na uongozi wa kipekee katika kusimamia amani, haki, haki za binadamu, usawa wa kijinsia, na uwezeshaji wa wanawake na wasichana," kulingana na Wizara ya Mambo ya Nje.

Agather Atuhaire, raia wa Uganda, alituza kwa kazi yake ya kutetea haki za binadamu na utawala wa sheria nchini Uganda.

Forum

XS
SM
MD
LG