Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 20, 2024 Local time: 19:45

Biden atumia hotuba ya 'Hali ya Taifa' kujipigia debe kuelekea uchaguzi wa Novemba


Rais wa Marekani Joe Bidenakilihutubia bunge mjini Washington.
Rais wa Marekani Joe Bidenakilihutubia bunge mjini Washington.

Rais wa Marekani Joe Biden alitumia hotuba yake ya Hali ya Taifa Alhamisi usiku kama jukwaa la kuwarai Wamarekani kumchagua kwa muhula wa pili, huku akimkosoa vikali mpinzani wake mkuu, mgombea wa chama cha Republikan, Donald Trump.

Biden alimkosoa rais huyo wa zamani kwa kile alichokiita kuunga mkono "chuki, kuwa na kisasi na kuhatarisha uhuru ndani na nje ya nchi.”

Mara kwa mara kwenye hotuba hiyo, Biden alimtuhumu "mtangulizi wangu" bila kumtaja Trump kwa jina, akipaza sauti yake huku akijaribu kutuliza wasiwasi wa wapiga kura kuhusu umri wake na utendaji wa kazi kwelekea kwa uchaguzi wa mwezi Novemba.

Akionekana mwenye ari na ukakamavu kuliko katika hotuba zake za hapo awali za Hali ya Taifa, Biden, mwenye umri wa miaka 81, alikosoa sera za Warepublikan, kuhusu uchumi, ushuru na huduma ya afya, kati ya mengine.

"Uhuru na demokrasia vinashambuliwa nyumbani na ng'ambo kwa wakati mmoja," Biden alisema alipokuwa akiwasihi wabunge kuunga mkono juhudi za Ukraine za kujilinda dhidi ya uvamizi wa Russia.

"Historia inatazama," alisema.

Biden alizungumza kuhusu vurugu za Januari 6, 2021 katika majengo ya bunge zilizofanywa na wafuasi wa Trump waliotaka kubatilisha uchaguzi wa 2020, na kutishia demokrasia.

"Mtangulizi wangu - na baadhi yenu hapa - mnataka kuuzika ukweli kuhusu Januari 6 - sitafanya hivyo," Biden alisema. "Huu ni wakati wa kusema ukweli na kuuzika uongo. Ukweli wa wazi ni kwamba huwezi kupenda nchi yako pale tu unaposhinda."

Rais Biden muda mfupi kabala ya kuanza hotuba ya Hali ya Taifa mwaka 2024.
Rais Biden muda mfupi kabala ya kuanza hotuba ya Hali ya Taifa mwaka 2024.

"Maisha yangu yamenifunza kukumbatia uhuru na demokrasia," Biden alisema. "Mustakabali unaotokana na maadili ya msingi ambayo ni kielellezo cha Marekani: uaminifu, adabu, utu, usawa. Kuheshimu kila mtu. Sasa baadhi ya watu wengine wa umri wangu wanaona hadithi tofauti. hadithi ya Marekani ya chuki, na kulipiza kisasi. Huyo siyo mimi," alisema mwansiasa huyo.

Biden alitetea mafanikio yake katika miundombinu na uzalishaji wa bidhaa, na kulitaka bunge kuidhinisha msaada zaidi kwa Ukraine, sheria kali za uhamiaji na bei ya chini ya dawa. Pia alijaribu kuwakumbusha wapiga kura juu ya hali aliyorithi alipoingia ofisini mnamo 2021.

Biden alielezea taswira ya mustakabali wenye matumaini kwa nchi huku sheria kubwa alizotia saini katika miaka yake miwili ya kwanza ofisini zikitekelezwa.

Trump, kwa upande wake, alisema alipanga kujibu matamshi ya Biden kwenye jukwaa matandao wake wa kijamii wa Truth Social.

Rais Biden amsalimia Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mike Johnson.
Rais Biden amsalimia Spika wa Baraza la Wawakilishi, Mike Johnson.

Awali, Biden alishutumu utawala wa Rais wa Russia Vladimir Putin kwa kuikadamiza Ukraine. Alisema ili Ukraine ifanikiwe inahitaji msaada wa Marekani na kuwa Marekani itasimama na nvhi hiyo.

Kuhusu suala la Vita vya mashariki ya Kati, Biden alisisitiza umuhimu wa kuundwa kwa mataifa mawili huru kama mojawapo ya suluhu ya kudumu.

Moja ya masuala makuu aliyoyazungumzia kwa muda ni hali ya uchumi, akieleza jinsi utawala wake ulivyobuni nafasi za ajira Millioni 15.

Wabunge wamshangilia Rais Biden wakati wa hotuba yake ya 'Hali ya Taifa' 2024.
Wabunge wamshangilia Rais Biden wakati wa hotuba yake ya 'Hali ya Taifa' 2024.

Biden pia aliangazia mafanikio yake katika "kurejesha uongozi wa Marekani kwenye jukwaa la dunia

Kabla ya hotuba yake kuanza waandamanji walikusanyika nje ya majengo ya bunge kumshinikiza Biden kuchukua hatua zitakazopelekea kusitishwa kwa mapigano katika Ukanda wa Gaza na kuruhusu msaada kuiingia.

-Mwandishi wa VOA Hubba Abdi pia alichangia ripoti hii.

Forum

XS
SM
MD
LG