Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 14:09

Trump na Harris waanza upinzani kuelekea Novemba


Kinyang’anyiro cha kuwania urais wa Marekani kimepata nguvu mpya Jumanne, wakati Rais wa zamani Donald Trump na mpinzani wake mpya wa Mdemokrat, Makamu wa Rais wa sasa wa Marekani, Kamala Harris, wakionyesha kutosita kurushiana vijembe wakielekea kwenye uchaguzi wa Novemba.

Wakati huo huo hapa Washington, Rais Joe Biden amerejea kimya kimya White House, baada ya kupona COVID-19, na kufikia matarajio kwamba atatumia muda wake uliobakia ofisini kufikia malengo ya sera za kigeni.

Kupitia mtandao wake wa kijamii Truth Social, Trump mwenye umri wa miaka 79, Jumanne amesema Kamala Harris huharibu kila kitu anachogusa, hapo awali, alimshutumu kwa kusaidia kuficha hali ya Biden.

Kwa upande wa makamu wa rais Kamala Harris, ambaye ni mwendesha mashitaka wa zamani wa jimbo lenye idadi kubwa ya watu California, amesema anayajua mapungufu ya Trump.

Mwishoni mwa mwezi Mei, Trump alipatikana na hatia kwa makosa 34 aliyoshitakiwa, pamoja na kudhalilisha wanawake.

Forum

XS
SM
MD
LG