Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Septemba 17, 2024 Local time: 14:57

Makamu wa Rais kuzindua uchaguzi wake kwa kumteua mgombea mwenza


Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris
Makamu wa Rais wa Marekani Kamala Harris

Makamu Rais wa Marekani, Kamala Harris ameripotiwa kuzindua uchaguzi wake kwa kumteua mgombea mwenza katika kinyang’anyiro cha urais 2024. 

Mgombea mwenza wake mpya atamtaja na kujiunga naye katika tukio la kampeni siku ya Jumanne huko Pennyslvania, wakati huo huo Rais wa zamani Donald Trump aliingia katika mtandao wa kijamii kuelezea kesi yake kwanini ni vyema kuwepo na mabadiliko kwa sehemu na tarehe ya mdahalo ujao wa wagombea urais.

Matarajio yanaongezeka kuhusu nani atakuwa Makamu Rais wa Marekani ambaye mgombea Urais wa Democratic Kamala Harris atamchagua kama mgombea mwenza wake katika uchaguzi wa rais mwaka 2024.

Washindani wa juu ni pamoja na Gavana wa Pennyslvania Josh Shapiro, Gavana wa Minnestoa Tim Walza na Seneta wa Marekani, Mark Kelly.

Kutoka kushoto: Seneta wa Marekani Mark Kelly, Gavana wa Minnesota Tim Walz, Gavana wa Pennsylvania Josh Shapiro
Kutoka kushoto: Seneta wa Marekani Mark Kelly, Gavana wa Minnesota Tim Walz, Gavana wa Pennsylvania Josh Shapiro

Mwanasayansi wa siasa katika chuo kikuu cha Duke, Jon Green ameiambia VOA kwa njia ya Skype kwamba uchaguzi wa Makamu Rais utakuwa kwa wapiga kura wa Marekani...

...na hisia kwa uamuzi wa Harris kuhusu uwezekano wa kuwa rais wa 47 wa Marekani.

Jon Green, Mwanasayansi wa Siasa anaeleza: “Inaashiria sana kuhusu yeye na vipaumbele vyake na mwelekeo wake wa utawala katika misingi ya nani atamuweka katika upande wake kwa sababu yoyote ile endapo hatakuwa na uwezo wa kufanya kazi na kutimiza majukumu yake kama rais.”

Harris anapanga kutembelea majimbo kadhaa yenye ushindani na Makamu Rais atakayemchagua kuanzia Jumanne huko Pennyslvania. Kampeni ya Trump pia ilitarajiwa kuendelea kuwekeza muda na nguvu katika majimbo ambayo huenda yakaamua matokeo ya uchaguzi mkuu wa Novemba.

Jon Green, Mwanasayansi wa Siasa anaeleza haya: “Wakati huu katika majimbo kama Pennsylvania, Wisconsin, Michigan, Arizona yote ni makubwa na yanaonyesha kuwa ushindani.”

Wakati wapiga kura wa Marekani wakisubiri tangazo la Makamu Rais wa Democrati kuna pia mtizamo mpya juu ya iwapo Harris atakuwa na mdahalo…

… hasimu wake wa kisiasa na Rais wa zamani Donald Trump. Mteule mgombea wa Republican anadai kwamba hivi sasa kwa vile Rais Joe Biden amejiondoa katika ushindani, mdahalo wa awaio uliopangwa kufanyika Septemba 10 kwenye ABC ni vyema uchukuliwe na Fox News in Pennsyvlania mapema mwezi Septemba, na kuwepo na watazamaji.

Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan Donald Trump
Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris na mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republikan Donald Trump

Siku ya Jumamosi Trump aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social “Nitaonana naye Septemba 4, au sitamuona kabisa.”

Kampeni ya Harris imekuwa kimya kama waendelee na mpango wa awali wa mdahalo.

Kamala Harris, Mgombea Urais wa Democratic anasema: “Ndiyo, Donald, natumaini utafikiria kukutana na mimi katika jukwaa la mdahalo kwasababu kama msemi unavyosema, kama una chochote cha kusema, niambie kwenye uso wangu.”

Iwapo Harris na Trump watakutana ana kwa ana hilo bado linasubiriwa kuonekana lakini rais wa zamani Trump atakuwa na fursa mpya kuelezea kasi yake dhidi ya Harris na mgomeba mwenza wake mpya.

…. atakapokuwa katika mikutano ya kampeni huko Bozeman, Montana Agosti 9.

Forum

XS
SM
MD
LG