Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 13:49

Uamuzi wa Rais Biden kujiondoa kuwania urais wawashangaza wengi


Rais wa Marekani Joe Biden
Rais wa Marekani Joe Biden

Uamuzi wa Rais Joe Biden siku ya Jumapili kujiondoa katika kuwania tena urais ulikuwa ni wa kushangaza huko White House na nje ya hapo, na kuacha hali ya kutokuwa na uhakika kuhusu uteuzi wa Democrati kufuatia hatua hiyo. 

Nini kitatokea sasa katika siasa za Marekani, baada ya Rais Joe Biden kufanya uamuzi wa kushtua siku ya Jumapili kwa kujiondoa katika kinyang’anyiro cha urais?

Jumatatu asubuhi, ilionekana kila mmoja alikuwa na nadharia yake.

Lakini Kwanza: baadhi wameangazia yale yaliyopita, kutoka kwa mtu ambaye hivi sasa atakuwa katikati ya jukwaa. Jumatatu, mgombea mwenza wa Biden, Makamu Rais Kamala Harris, alijitokeza na kutoa tangazo lake la kwanza, alipokuwa akiwa mwenyeji wa wanariadha katika tukio lililofanyika White House.

Amesema Biden, ambaye anapata nafuu kutokana COVID 19 nyumbani kwake huko Delaware na hajaonekana hadharani tangu wiki iliyopita, anaendelea kupata ‘afueni kwa haraka.’

Kamala Harris, Makamu Rais anasema: “Urithi wa historia ya Joe Biden katika muda wa miaka mitatu iliyopita hauwezi kulinganisha na historia ya sasa. Katika awamu moja, tayari amevuka yaliyofanywa na marais wengi ambao walihudumu kwa awamu mbili.”

Makamu wa Rais Kamala Harris akiwa katika mkutano wa kampeni huko Milwaukee, Wisconsin Julai 23, 2024.
Makamu wa Rais Kamala Harris akiwa katika mkutano wa kampeni huko Milwaukee, Wisconsin Julai 23, 2024.

Lakini wakosoaji wa Biden wa Republican wanahoji iwapo abakie madarakani kama rais.

Mbunge Mike Johnson, Spika wa Bunge anasema: “Kama mtu yeyote atakiri kuwa hana uwezo wa kuendesha kampeni, ni dhahiri hana uwezo wa kuendesha nchi.”

Wafuasi wana hamasa kubwa, huku Wademocrat wa juu wakijipanga nyuma ya Harris.

Mbunge Adam Schiff, Mdemocrat anaeleza: “Nina imani kubwa kwamba anaweza kumshinda Donald Trump. Nina hamasa jinsi haraka watu walivyokuja pamoja kuunga mkono ugombea wake.”

Kwahiyo kitu gani kinatokea sasa? Kwanza, kanusho:

Peter Loge, Chuo Kikuu cha George Washington anasema: “Utafaiti umebaini kwamba wachambuzi wa siasa si wazuri katika kutabiri matokeo ya kisiasa kuliko wale wanaorusha kete. Kwahiyo, nitachukua chochote ambacho mtu yeyote kama mimi anasema kwa kuangalia kwa umakini mkubwa sana.”

Wanahistoria wamepuuza wazo kwamba matuko haya ya kushangaza huenda yakasababisha ukosefu wa uthabiti.

Thomas Schwartz, Chuo Kikuu cha Vanderbilt anaeleza: “Nadhani White House ni mashine kubwa sana kuliko rais mwenyewe. Kwa kweli, atakuwa kama rais ambaye hawezi kufanya mengi kwa muda uliobaki, tumekuwa na marais kama hao katika siku zilizopita, na hilo kwa kweli si suala na wala hakuna hatari yoyote.”

Baadhi ya wachambuzi wanasema, kwamba kwa kiasi fulani, hii inafanya uchaguzi kuwa rahisi zaidi.

William Galston, Taasisi ya Brookings anasema: “Kunatakuwa na mgawanyiko wa majukumu. Atakuwa rais. Kamala Harris atakuwa mgombea, na hili linafanya iwe rahisi kwa wote kwa njia fulani kwasababu kila mtu atakuwa na kazi tofauti.”

Ambayo italeta swali kubwa kuliko yote, ambalo kila mpiga kura wa Marekani anaweza kujibu, ni Novemba: nani anatakiwa kwenda kuishi White House kwa miaka minne?

Forum

XS
SM
MD
LG