Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:31

Wademokrat wadai kujiandaa kumshambulia Trump kwa umri wake


Mgombea wa urais wa Chama cha Republican Donald Trump ( katikati)
Mgombea wa urais wa Chama cha Republican Donald Trump ( katikati)

Wademokrat wako tayari kugeuza udhaifu wa kisiasa ambao ulikuwa ukimsakama Biden—Umri wake – na kumshambulia Trump.

Hii pengine inawezekana kuwa na athari kwa Donald Trump, ambaye ndiye mgombea mwenye umri mkubwa sana katika historia ya Marekani, dhidi ya Kamala Harris,” amesema Mwakilishi Maxwell Frost mwenye umri ya miaka 27 kutoka chama cha Domokratic Florida ambaye amekuwa akifanya kazi kuwafikia wapiga kura vijana katika kampeni ya Biden.

Frost ambaye anamuunga mkono Harris, alizungumzia kazi ya makamu wa rais kuhusu ulinzi wa ghasia za bunduki kama suala ambalo linaweza kuwahusisha vijana wapiga kura na kusema kuwa “ataweza kushinda tena kura za vijana wengi.”

“Ni mtu anayethamini sauti za vijana kwa ujumla,” alisema.

Trump anataka kufanya mdahalo wa pili wa urais utakaofanyika katika kituo cha television cha FOX, ambacho kinaonaekana kuwa rafiki kwake, badala ya ABC katika kipindi hichi ambacho Biden amejiondoa.

Wakati huo huo Makamu wa rais Kamala Harris kupitia ukurasa wake wa X aliandika “Kwa niaba ya Wamarekani, ninamshukuru Joe Biden kwa uongozi wake mzuri kama rais wa Marekani, kwa miongo kadhaa ya uongozi wa nchi yetu. Nimefurahi kuungwa mkono na rais na nia yangu ni kupambana na kushinda uteuzi huu.”

Naye rais zamani wa Marekani Barack Obama kupitia ukurasa wake wa X amemuelezea Biden kuwa ni mmoja wa marais waliofanya mambo mengi, pamoja na kuwa rafiki mkubwa na mshirika wake.

“Leo tumekumbushwa – tena - kwamba yeye ni mzalendo wa hali ya juu,” aliandika.

Forum

XS
SM
MD
LG