Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:42

China yakataa kutoa maoni kuhusu Biden kujiondoa katika kinyang’anyiro cha urais


Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) na rais wa China Xi Jinping (Kushoto) huko Beijing Agosti 18, 2011. Picha na REUTERS/Lintao Zhang/Pool
Rais wa Marekani Joe Biden (kulia) na rais wa China Xi Jinping (Kushoto) huko Beijing Agosti 18, 2011. Picha na REUTERS/Lintao Zhang/Pool

Wizara ya mambo ya nje ya China siku ya Jumatatu ilisema haina maoni yoyote kuhusu kujiondoa kwa rais wa Marekani Joe Biden katika Kinyany’anyiro cha urais, ikisema kuwa “uchaguzi huo wa rais unaihusu Marekani yenyewe.”

Shirika rasmi la habari la Xinhua, hata hivyo lilitoa maoni kwamba “kwa mara nyingine tena hatua hiyo imefichua siasa chafu za Marekani”

“Kujiondoa kwa Biden kwa mara nyingine tena kunafichua vurugu na mwelekeo wa siasa za Marekani ambapo maslahi ya siasa zinazoegemea upande mmoja yanatawala na pesa kuendesha uchaguzi” Xinhua ilisema katika uhariri.

Wakati huo huo siku ya Jumatatu gavana jimbo la Maryland Wes Moore, gavana wa Michigan Gretchen Whitmer, gavana wa Illinois Gov. J.B. Pritzker na gavana wa Kentucky Andy Beshear, wamemuunga mkono Kamala Haris na kufanya idadi ya wapinzani wakuu dhidi ya makamu huyo wa rais kuwa ndogo wakati akielekea kujipatia wajumbe watakaompigia kura katika kampeni yake ya kwenda White House.

Kushinda uteuzi ni hatua ya kwanza kwenye orodha ya mambo ya kisiasa kwake baada ya uamuzi wa Biden wa kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho, ambapo Haris alifahamu siku ya Jumapili asubuhi alipokuwa kwa njia ya simu na rais huyo.

Endapo akifanikiwa kupata uteuzi, hana budi kuchagua mgombe mwenza na aanzishe operesheni kubwa ya kisiasa ili kuongeza uwakilishi wake badala ya wa Biden akiwa na zaidi ya siku 100 zimebaki kabla ya uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG