Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Desemba 22, 2024 Local time: 20:59

Biden aelezea sababu za kujiondoa kuwania urais kwa Wamarekani


Rais wa Marekani Joe Biden akihutubia taifa kuhusu uamuzi wake wa kujiondoa kuwania urais katika uchaguzi wa Novemba,White House mjini Washington, Juai 24, 2024.
Rais wa Marekani Joe Biden akihutubia taifa kuhusu uamuzi wake wa kujiondoa kuwania urais katika uchaguzi wa Novemba,White House mjini Washington, Juai 24, 2024.

Rais wa Marekani Joe Biden amesema "anapitisha mwenge kwa kizazi kipya" alipokuwa akielezea uamuzi kuondoka kwake ghafla kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa rais wa 2024.

Amesema hayo kwa Wamarekani kwa mara ya kwanza Jumatano usiku, katika hotuba yake kutoka ofisi ya White House, maarufu kama Oval Office, iliyohitimisha zaidi ya miaka 50 katika siasa.

"Ninaheshimu ofisi hii," Biden alisema. "Lakini naipenda nchi yangu zaidi."

Biden, mwenye umri wa miaka 81, kwa wiki kadhaa alikuwa amekataa shinikizo kutoka kwa wademokrat wenzake, la kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho

Kufuatia kile kilichoelezwa kwama kutofanya vyema katika mjadala kati yake na rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, uliofanyika Juni 27, akisema wakati mmoja ni "“Mwenyezi Mungu" pekee ndiye anayeweza kumshawishi aondoke.

“Nimeamua njia bora ni kuupitisha mwenge kwa kizazi kipya. Hiyo ndiyo njia bora ya kuunganisha taifa letu," Biden alisema.

Biden ameshatangaza kwamba anamuunga mkono makamu wake, Kamala Harris, mwenye umri wa miaka 59, kuwa mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Democratic.

Mwansiasa huyo mkongwe anaungana na James K. Polk, James Buchanan, Rutherford B. Hayes, Calvin Coolidge na Harry Truman kama marais ambao wote waliamua kutogombea muhula wa pili.

Forum

XS
SM
MD
LG