Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 19:13

Biden alenga marekebisho kwenye Mahakama ya Juu ya Marekani


Jengo la Mahakama Kuu ya Marekani, Washington DC.
Jengo la Mahakama Kuu ya Marekani, Washington DC.

Rais wa Marekani Joe Biden amezindua pendekezo lililosubiriwa kwa muda mrefu la kufanya marekebisho kwenye Mahakama ya Juu ya Marekani.

Kiongozi huyo mdemokrat analiomba bunge kuweka muda wa kuhudumu , pamoja na kanuni za utenda kazi kwa majaji tisa wa mahakama hiyo. Biden pia anawaomba wabunge kufanya marekebisho ya katiba yatakayoweka kiwango kwa haki ya kutoshitakiwa kwa rais.

Ikulu ya Marekani Jumatatu imeelezea kwa kina kuhusu pendekezo la Biden, ambalo huenda lisipitishwe kutokana na migawanyiko bungeni, ikiwa zimebaki siku 99 kabla ya uchaguzi mkuu wa Novemba. Hata hivyo wademokrat wanaamini kuwa pendekezo hilo litawavutia wapiga kura wanapofanya maamuzi yao kuelekea uchaguzi huo.

Mgombea urais mtarajiwa wa chama cha Demokrat ,makamu wa rais Kamala Harris, analenga kufanya kampeni zake dhidi ya mrepablikan Donald Trump, kwa kuwaeleza wapiga kura wachague kati ya “uhuru au ghasia.” Ikulu ya Marekani inalenga kushugulikia ghadhabu miongoni mwa wademokrat kuhusu Mahakama ya Juu yenye wingi wa wakonsevative 6-3, kutokana na kubatilisha sheria muhimu za utoaji mimba, pamoja na nguvu za serikali kuu ambazo zimekuwepo kwa miongo kadhaa.

Forum

XS
SM
MD
LG