Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 08:12

Vifo katika ajali ya migodi haramu Indonesia vyafikia 16


Ajali ya migodi baada ya wachimbaji kufukiwa na vifusi kufuatia maporomoko ya miamba na michanga. Waokoaji wakiwa katika operesheni ya uokoaji katika mlima wa Bolaang Mongondow, Kaskazini mwa Sulawesi, Indonesia, Jumanne, Machi 5, 2019.
Ajali ya migodi baada ya wachimbaji kufukiwa na vifusi kufuatia maporomoko ya miamba na michanga. Waokoaji wakiwa katika operesheni ya uokoaji katika mlima wa Bolaang Mongondow, Kaskazini mwa Sulawesi, Indonesia, Jumanne, Machi 5, 2019.

Idadi ya vifo kufuatia ajali katika machimbo ya migodi kaskazini mwa Indonesia imeongezeka Jumatano na kufikia watu 16 huku matumaini ya kupata manusura yakiendelea kufifia.

Watu 18 wameokolewa wakiwa na majeraha mabaya, kutoka kwa machimbo ya migodi haramu kwenye kisiwa cha Sulawesi.

Baadhi ya mashirika ya uokoaji yameripoti kwamba huenda kulikuwa na wachimba migodi kati ya 50 na 100 wakati ajali ilipotokea na maafisa wamefutilia mbali matumaini ya kuwapata waathiriwa wote.

Haijulikani ni wachimba migodi wangapi walikuwa ndani ya machimbo hayo wakati ajali hiyo ikitokea, Jumanne wiki iliyopita.

Juhudi za uokoaji zimetatizwa na hali ya mwinuko wa ardhi, udongo mwepesi na machimbo hatari ya madini ambayo ni membamba.

Msemaji wa idara ya majanga ya Indonesia Sutopo Purwo Nugroho amesema maafisa wa uokoaji wamekuwa wakifanya kazi masaa 24 tangu Jumatatu, sehemu hiyo baada ya kupewa taarifa kwamba ni eneo salama kuendelea operesheni hiyo ya uokoaji.

Visa vya ajali katika machimbo ya madini haramu, huripotiwa kila mara nchini Indonesia, yenye utajiri mkubwa wa madini.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG