Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:02

Indonesia : Idadi ya walio kufa katika janga la tsunami yafikia 400


Wakazi walioathiriwa na janga la tsunami wakihudhuria maombi siku ya Krismasi katika kanisa la Carita Pentecostal huko Pandeglang, Jimbo la Banten, Indonesia, Disemba. 25, 2018.
Wakazi walioathiriwa na janga la tsunami wakihudhuria maombi siku ya Krismasi katika kanisa la Carita Pentecostal huko Pandeglang, Jimbo la Banten, Indonesia, Disemba. 25, 2018.

Idadi ya vifo kutokana na Tsunami iliyo tokea Jumamosi imefikia watu 400, wakati watu 1485 wakiwa wamejeruhiwa na wengine 154 hawajulikani waliko.

Wafanyakazi wa kutoa msaada nchini Indonesia, wameonya kwamba kuna uhaba wa maji safi na madawa kwa maelfu ya wale walioathiriwa na tsunami iliyo sababishwa na mlipuko wa volcano, katika pwani ya nchi hiyo.

Wasiwasi umeongezeka kuhusu uwezekano wa kulipuka magonjwa, waathiriwa wakilazimika kuishi katika kambi za muda.

Kwa mujibu wa ripoti za madaktari, idadi kubwa ya watoto wanaugua homa na kuumwa kichwa, bila ya kunywa maji wala kula chakula cha kutosha.

Tetemeko la ardhi lilofuatiwa na mawimbi makubwa yenye nguvu (Tsunami) iliifunika pwani ya Indonesia na kusababisha uharibifu mkubwa kusini mwa Sumatra na magharibi Java.

Makaazi yaliyo karibu na pwani, pamoja na hoteli za watalii ziliharibiwa vibaya.

Tukio la jumamosi halikuwa limetabiriwa na wataalam sasa wanaonya kwamba matukio Zaidi ya tsunami yanatarajiwa kutokea Indonesia.

XS
SM
MD
LG