Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 06:33

Idadi ya walio kufa Indonesia yafikia 373


Moshi mkubwa unaotokana na mlipuko wa volkano nchini Indonesia, Disemba. 23, 2018.
Moshi mkubwa unaotokana na mlipuko wa volkano nchini Indonesia, Disemba. 23, 2018.

Idadi ya walio kufa kutokana na tsunami nchini Indonesia imeongezeka kufikia 373 Jumatatu, kwa mujibu wa maafisa wanaosimamia maafa.

Watu wasio pungua 1,459 wameripotiwa kujeruhiwa na zaidi ya watu 100 hawajulikani waliko, Bodi ya Taifa ya Kusimamia Maafa Indonesia (BNBP) imesema Jumatatu – ikiwa takriban siku mbili kamili baada ya janga la tsunami kutokea kaitka pwani ya jimbo la Banten.

Zaidi ya majengo 1,000, zikiwemo nyumba 681, zimeharibiwa, na baadhi ya sehemu za eneo la Sunda Straits zimeendelea kukabiliwa na ukosefu wa umeme Jumatatu usiku, kwa mujibu wa BNBP.

Rais wa Indonesia Joko Widodo ametembelea baadhi ya maeneo uharibifu huo ulipotokea Jumatatu, akitembelea Hoteli ya Mutiara iliyoko katika ufukwe wa Carita jimbo la Banten.

Idara ya hali ya hewa, na Idara ya jiolojia (BMKG) iliripoti mlipuko wa volcano mnamo saa tatu usiku Jumamosi na tsunami ilipiga muda mfupi baada ya tangazo hilo, kiasi cha saa tatu na nusu usiku.

XS
SM
MD
LG