Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 20:55

Kifaa cha kurekodi sauti cha ndege ya Indonesia iliyopata ajali chapatikana


Lion Air Jetliner
Lion Air Jetliner

Maafisa wa serikali ya Indonesia wamesema kikosi kazi maalum kimefanikiwa kukipata kifaa kinacho rikodi sauti za marubani wakati ndege inaporuka ambacho kilikuwa kwenye ndege ya Lion Air Jetliner ambayo ilianguka katika bahari ya Java Octoba 2018, na kuuwa abiria wote 189 na wafanyakazi walio kuwa ndani yake.

Wazamiaji wa jeshi la majini walikipata kifaa hicho Jumatatu, siku kadhaa baada ya wazamiaji hao kupata ishara hafifu za mawasiliano kutoka katika kifaa hicho, ambacho kilikuwa kimezama mita kadhaa katika kina kirefu chini ya bahari kwenye matope.

Pande zote mbili za maafisa wa jeshi na raia ambao walihusika na zoezi hilo la kutafuta kifaa hicho wamesema kuwa mabaki ya binadamu yalipatikana karibu na kifaa hicho cha kurikodi sauti.

Kupatikana kwa kifaa hicho cha pili cha kurikodi sauti maarufu kama “black boxes” kinaweza kuwapa taarifa zaidi juu ya sababu zilizo fanya ndege hiyo ya aina ya Boeing 737 Max 8 Jet kuanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa ndege wa Jakarta hadi kisiwa kilicho kuwa karibu cha Bangka-Belitung. Kifaa cha kurikodi takwimu za ndege kilipatikana siku kadhaa baada ya ajali hiyo.

Wachunguzi walioko katika kamati ya usalama wa usafiri wa taifa wametoa ripoti ya awali Novemba inayo tokana na taarifa iliyo patikana kutoka katika kifaa kinacho rikodi takwimu za ndege ambacho ni mfumo unao jitegemea wa usalama wa ndege ambao ulikuwa unaisukuma ndege hiyo kushuka chini, pamoja na juhudi zilizo gonga ukuta za marubani kujaribu kuiokoa ndege hiyo isianguke.

XS
SM
MD
LG