Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 09:40

Indonesia yatahadharisha juu ya mlipuko mpya wa volcano


Jivu linalotokana na mlipuko wa volcano katika mlima wa Anak Krakatau Indonesia.
Jivu linalotokana na mlipuko wa volcano katika mlima wa Anak Krakatau Indonesia.

Maafisa wa huduma za dharura Indonesia wameonya na kuongeza kiwango cha hatari ya mlipuko wa volcano katika mlima wa Anak Krakatau.

Mlipuko huo mapema wiki iliyopita uliopelekea mawimbi makubwa ya uharibifu kutokana na tsunami kupiga katika pwani ya magharibi ya nchi hiyo ambayo na kuuwa watu wapatao 430.

Maafisa wa dharura wameweka onyo la watu kutokaribia eneo la mlima huo wa Anak Krakatau ambao unaonekana utaripuka tena wakati wowote.

Vyanzo vya habari vimesema onyo la pili linalotahadharisha mlipuko huo wakati mlima huo ukiendelea kutoa gesi ya moto na volcano nyingine kwenye bahari pamoja na wingu zito la majivu angani.

Maafisa wameongeza eneo la kuzunguka volcano limefikia kilometa 5 wakati harakati za milipuko zikiendelea na mawimbi makubwa ikiashiriia kwamba mawimbi mengine makubwa zaidi ya uharibifui yanaweza kupiga.

Maafisa wa mamklaka ya usafiri wa anga wameonya ndege zisiruke kuelekea katika eneo hilo.

XS
SM
MD
LG