Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 02:59

Trump ashutumiwa kujaribu kuingilia kati uchaguzi wa Uingereza


Kiongozi wa chama cha Brexit Nigel Farage.
Kiongozi wa chama cha Brexit Nigel Farage.

Tuhuma za jaribio la kuingilia kati uchaguzi wa nchi nyingine zinaelekezwa dhidi ya Rais wa Marekani Donald Trump baada ya kufanya mazungumzo ya simu na radio moja ya Uingereza Alhamisi.

Wakati wa mazungumzo akiwa hewani na kiongozi wa Chama cha Brexit Nigel Farage, Trump alimpongeza Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson kuwa ni mtu barabara ambaye “ndiye mtu sahihi kwa nyakati hizi.”

Trump alimtaka Farage kushirikiana na Johnson, kiongozi wa Chama cha Waconservative, katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika Disemba 12, ambapo suala nyeti ni la Brexit.

“Iwapo yeye na wewe mtashirikiana, unajua kuwa ni nguvu isiyoweza kuzuilika [katika uchaguzi],” Trump alitamka hilo kupitia Radia LBC.

Farage, ambaye alikampeni kwa ajili ya kuwepo kura ya maoni mwaka 2016 kutaka msimamo wa wananchi iwapo Uingereza ijitoe Umoja wa Ulaya, ni mgombea katika uchaguzi ulioitishwa mapema kama kiongozi wa chama chake.

Kampeni za uchaguzi nchini Uingereza bado hazijaanza rasmi. Takwimu za utafiti wa hivi karibuni zinaonyesha chama cha Tories cha Johnson kikiongoza na chama cha Labour kikiwa nyuma yao, na pia chama cha Liberal Demokrats. Chama cha Farage cha Brexit kikochini katika kura na hivi sasa hakina uwakilishi katika Bunge la Uingereza.

Baadhi ya wachambuzi wa kisiasa, hata hivyo, wanaona matokeo ya uchaguzi huu hautabiriki, wakati chama cha Farage kikiwa na uwezo wa kugawanya kura ya Brexit na kuwaacha chama cha Conservative bila ya wingi wa kura.

Amkosoa kiongozi wa chama cha Labour

Mahojiano ya Rais wa Marekani Alhmaisi na Farage, yalipelekea kumkosoa kiongozi wa chama cha Labour, wakisema Jeremy Corbyn atakuwa “siyo mtu barabara kwa nchi yako” iwapo atachaguliwa kuwa waziri mkuu.

Corbyn mara moja alituma ujumbe wa Tweet akimshutumu Trump kwa “ kujaribu kuingilia kati uchaguzi wa Uingereza kumsaidia rafiki yake Boris Johnson kushinda uchaguzi.”

Mwandishi wa kisiasa wa gazeti la The Guardian, Andrew Sparrow, pia alisema Trump alitumia mahojiano hayo na Farage “kuingilia kati uchaguzi wa Uingereza.”

XS
SM
MD
LG