Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:35

Waziri Mkuu wa Uingereza aitisha uchaguzi mapema kukabiliana na upinzani


Waziri Mkuu Boris Johnson akizungumza baada ya matokeo ya kura katika Bunge Septemba 3, 2019, Picha kutoka REUTERS - RC11A5310AF0
Waziri Mkuu Boris Johnson akizungumza baada ya matokeo ya kura katika Bunge Septemba 3, 2019, Picha kutoka REUTERS - RC11A5310AF0

Wabunge wa upinzani Uingereza wanatarajiwa kupeleka muswada Jumatano kuchelewesha tena Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya (EU) ili kufikia makubaliano mapya ya namna ya kutoka katika umoja huo.

Waziri Mkuu Boris Johnson, ambaye ameahidi kukamilisha Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya ifikapo Octoba 31 bila ya kujali iwapo kuna makubaliano au la, amesema hatua iliyochukuliwa na bunge inamwacha akiwa hana chaguo ila kuitisha uchaguzi mapema.

Wabunge walioasi wanaweza kuchukua hatua baada ya kushinda kura 328 kwa 301 zilizopigwa Jumanne katika Bunge la Uingereza na hivyo kuweza kudhibiti suala la kujitoa Umoja wa Ulaya.

Wale wanaopinga kujitoa katika umoja huo bila ya makubaliano wanasema iwapo Johnson akiendelea na msimamo wake bila ya kufikia makubaliano katika kujitoa Umoja wa Ulaya, italeta maafa makubwa katika uchumi wa Uingereza.

Wabunge walioasi ni pamoja na wanachama kutoka chama cha upinzani na chama chake Johnson cha Conservative.

Wabunge wa Conservative Philip Lee kwa vituko alihama chama chake na kwenda upande wa upinzani Jumanne, akisema serikali “inafuata njia ya uharibifu katika kujiondoa Brexit bila ya kuwepo misingi yoyote,” ikihatarisha maisha na vipato vya watu.

XS
SM
MD
LG