Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:53

Mahasimu wa May waonya kupinga makubaliano mapya ya Brexit


Wanaopinga na kuunga mkono makubaliano ya Brexit wakiandamana nje ya Bunge la Uingereza, London, Septemba 5, 2018.
Wanaopinga na kuunga mkono makubaliano ya Brexit wakiandamana nje ya Bunge la Uingereza, London, Septemba 5, 2018.

Ilikuwa imewachukuwa viongozi 27 wa Umoja wa Ulaya na Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May dakika 40 tu kusaini makubaliano ya Uingereza kujitoa EU (Brexit) baada ya miaka miwili ya majadiliano magumu, lakini majaribio hayo na matatizo ya Uingereza kujitoa yaliyopitishwa Jumapili huko Brussels bado yako mbali kabisa kufikiwa.

Wakati wakipitisha mkataba huo wenye kurasa 585, na kurasa 26 zenye kuambatana na matamko ya kisiasa ambayo yanatoa mipaka ya mazungumzo juu ya uwezekano wa makubaliano ya biashara huru kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya, wapinzani wenye nguvu London wametengeneza mikakati ya kuharibu makubaliano hayo.

Kuna ushahidi mdogo sana kwamba waziri mkuu aliyeko tayari mashakani atakuwa na uungwaji mkono wa kutosha kushinda sheria inayopitishwa na bunge la Uingereza juu ya makubaliano hayo mwezi ujao.

Hilo lilikuwa liko wazi wa maafisa wa Kamisheni ya Ulaya Jumapili wakati viongozi wa EU walipounga mkono juu ya matakwa ya Uingereza kujiengua kutoka Umoja huo waliokuwa wanachama kwa miaka 44.

Rais wa Tume ya EU Jean Claude Juncker aliishauri kuwa Uingereza isitegemee kupata makubaliano bora zaidi, iwapo bunge lake linapinga mkataba huo. “Huu ni wakati kila mtu achukuwe majukumu yake,” amesisitiza.

Haya ni makubaliano, ni makubaliano bora kuweza kufikiwa na EU haitabadilisha misimamo wake wa msingi linapokuja suala hili, kwa hivyo nafikiri bunge la Uingereza - kwa kuwa ni bunge lenye busara - litapitisha makubaliano haya," ameongeza

Waziri Mkuu wa Holand Mark Rutte amewashauri wabunge wa Uingereza kuwa hakuna makubaliano bora zaidi yanayoweza kutolewa kutoka Umoja wa Ulaya, bila ya kukubaliana na mkataba huo.

XS
SM
MD
LG