Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:11

May aahidi kuunda serikali na Foster


Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May

Theresa May anatarajiwa kuunda serikali itakayo lipeleka taifa mbele siku zijazo, akiungwa mkono na chama cha DUP.

May alisema hayo baada ya kutembelea ikulu ya Buckingham, na kuongeza kuwa chama chake tu (Conservative) ndio kina "uhalali" wa kutawala, pamoja na kushindwa kupata wingi wa wabunge katika uchaguzi wa Alhamisi.

Alisema angeweza kujiunga na "rafiki" zake wa Chama cha DUP na "kufanya kazi" inayohusiana na Brexit.

Kwa mujibu wa idhaa ya BBC wanachama wa chama cha labour walisema wao ndio "washindi halisi" huku wanademokrasia huria wakisema Bi May unapaswa kuwa na "aibu" ya kuendelea na kazi.

Akizungumzia "uhusiano imara" aliokuwa nao na DUP lakini akitoa maelezo kidogo ya jinsi mpangilio wao unaweza kufanya kazi, alisema serikali itaweza "kuongoza nchi katika mazungumzo muhimu ya Brexit" yanayofaa kuanza katika muda wa siku 10 tu.

Kiongozi wa DUP Arlene Foster alithibitisha kwamba amezungumza naye Bi May na kuwa watawasiliana zaidi ili "kujadili jinsi wataweza kuleta utulivu kwa taifa, wakati huu wa changamoto kubwa".

Licha ya kuwa wanafanya bidii siku zote kwa ajili ya "mpango bora" kwa Ireland ya Kaskazini na watu wake, alisema chama chake daima kinataka manufaa yaliyo bora kwa Uingereza kwa jumla.

Baada ya matokeo ya maeneo mengi kutangazwa, Theresa May alipungukiwa na wabunge 12 ukilinganisha na wabunge aliokuwa nao wakati wa kuitisha uchaguzi huo.

Kiongozi wa chama cha Leba Jeremy Corbyn amesema pia kwamba yuko "tayari kutumikia" taifa na kuwa chama chake kinamahusiano mazuri na chama cha May.

"Vyama vyetu viwili vimekuwa na uhusiano bora kwa miaka mingi," alisema.

"Na hii inanipa mimi imani ya kwamba tutaweza kufanya kazi pamoja kuboresha maslahi ya Uingereza."

XS
SM
MD
LG