Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:41

Trump aishinikiza Qatar, huku Tillerson akitafuta ufumbuzi


Rais Donald Trump
Rais Donald Trump

Rais Donald Trump Ijumaa amezidi kuikosoa Qatar, nchi ndogo ya Ghuba inayokabiliwa na mgogoro wa kidiplomasia na jirani zake wa nchi za Kiarabu.

“Nchi ya Qatar, kwa bahati mbaya ina historia ya kufadhili makundi ya kigaidi katika daraja ya juu,” Trump amesema hayo katika mahojiano na waandishi kwenye bustani ya Rose Garden.

Maoni ya Trump yamekuja dakika chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje Rex Tillerson alipotoa wito wa kuwepo utulivu na kuondolewa vikwazo vilivyowekwa dhidi ya Qatar na Jirani zake.

Tillerson amesema vizuizi hivyo vinasababisha matatizo “yasiokusudiwa” ya kibinadamu na biashara na inazuia Jeshi la Marekani kuendesha shughuli zake katika eneo la Mashariki ya Kati na pia kampeni ya kuitokomeza kikundi cha ISIS,” au Kikundi cha Kigaidi cha Islamic State.

Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu, Bahrain na Misri wiki hii viliiwekea vikwazo vya kiuchumi na kidiplomasia Qatar, katika hali ilioendelea kuwa ngumu kutokana na mgogoro unaoendelea kwa muda mrefu katika eneo hilo.

Nchi hizi, na hasa Saudi Arabia, hazikubaliani na Qatar juu ya suala la vikundi vya Kiislam, kama vile Muslim Brotherhood, na Iran.

Marekani imetumia umakini wa kidiplomasia katika mgogoro huu, ikiegemea pande zote mbili; Saudi Arabia and Qatar. Qatar ni mwenyeji wa kituo kikubwa cha kijeshi cha Marekani katika Mashariki ya Kati, kinachofanya mapambano dhidi ya Kikundi cha IS.

Kwa upande wake Trump katika hali isiyo ya kawaida hakusita kuikosoa kwa nguvu zote Qatar. Mapema wiki hii, Trump ametuma mtiririko wa ujumbe wa tweets akionyesha kufurahia,na pia kujigamba kwa hatua hiyo, kwa Qatar kutengwa na nchi hizo za Kiarabu.

XS
SM
MD
LG