Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:17

Hatma ya Brexit : Wananchi wakerwa na msimamo wa viongozi wa kisiasa Uingereza


Wananchi wajitokeza kupinga Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya nje ya Bunge la Uingereza, London Machi 12, 2019.
Wananchi wajitokeza kupinga Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya nje ya Bunge la Uingereza, London Machi 12, 2019.

Wananchi wa Uingereza wamesikitishwa na viongozi wao wa kisiasa kushindwa kufikia muwafaka katika suala zima la Uingereza kujiondoa katika Umoja wa Ulaya (EU).

Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema kuwa hadi sasa wananchi wako njia panda juu ya hatma ya Brexit.

Wamesema kuwa kumekuwa na upinzani mkubwa kati ya wanasiasa hao juu ya mpango wa Theresa May unaotaka Uingereza kujiondoa EU.

Tamati ya siku 17

Wabunge kwa mara ya pili Jumanne wamepinga suala hilo la kujiondoa huku zikiwa zimesalia siku 17 hadi muda wa taifa hilo kujitoa umoja huo.

May, amesema anasikitika sana kutokana na hatua ya bunge kuyakataa makubaliano yake yakujiondoa Umoja wa Ulaya- EU kwa mara ya pili na kuiweka nchi hiyo katika mgogoro mbaya zaidi wa kisiasa uliyowahi kuikumba nchi hiyo, zikiwa zimebakia siku 17 kabla ya tarehe ya mwisho ya kujiondoa kutoka umoja huo.

Wabunge waliopiga kura ya hapana

Wabunge 391 walipiga kura kukataa mkabata wa Theresa May uliyokuwa umefanyiwa marekebisho huku juhudi zake za mwisho za kufanya mazungumzo na wakuu wa EU Jumatatu kukabiliana na wakosoaji wake, kugonga ukuta.

Kadhalika wabunge 242 pekee ndio waliounga mkataba wake May. May amesema kwamba kwa sasa, bunge la Uingereza sasa halijui cha kufanya kati ya kubatilisha kipengele cha50 kinachoelezea azma yakujiondoa EU, kuitishakura ya pili ya maoni au kuendelea na mkataba na sio mkataba uliopo.

Thamani ya sarafu yashuka

Thamani ya sarafu ya Sterling imeanguka kwa asilimia 2 kutoka dola 1.3086 hadi 1.3005, muda mfupi baada ya kura iliyopigwa na bunge la nchi hiyo.

Wabunge wa Uingereza wanatarajiwa kupiga kura Jumatano kuamua iwapo Uingereza ijiondoeEU na makubaliano au bila ya makubaliano yoyote.

Fursa nyingine

Iwapo watapiga kura kupinga mkakati huo, watapiga tena kura siku inayofuata kuidhinisha iwapo kurefushwa kwa kipengere cha kifungu namba 50 - mfumo wa sheria utakao iondoa Uingereza katika EU kufikia Machi 29.

May amesema wabunge watalazimika kuamua iwapo wanataka kuahirisha Brexit, kuandaa kura nyingine ya maoni au iwapo "wanataka kuondoka na mkakati mpya.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG