Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:34

Kura ya kutokuwa na imani na Theresa May haikuzaa matunda


Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May
Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alishinda kura za wa-Conservative 200 dhidi ya 117 katika bunge la uingereza na kuendelea na wadhifa wake

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May alinusurika kura ya kutokuwa na Imani naye na hivyo kuendelea na wadhifa wake na kuzuia changamoto nyingine kwa uongozi kwa mwaka mmoja. May alishinda kura za wa-Conservative 200 dhidi ya 117 katika bunge la uingereza jana Jumatano.

Katika mkutano wa faragha na wabunge wa-Conservative kabla ya kura kuanza, May alisema atajiuzulu kama kiongozi wa Uingereza kabla ya uchaguzi uliotarajiwa kufanyika 2022 hatua ambayo huwenda imemsaidia kupata uungaji mkono wa baadhi ya wabunge ambao walikuwa hawajafanya maamuzi wakati wanakwenda kupiga kura ya siri. Tangazo la May la kutowania kuchaguliwa tena lilithibitishwa na waziri katika baraza la mawaziri, Amber Rudd na wabunge wa-conservative Alec Shelbrooke na Robert Buckland.

Mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Labor Party, Ian Lavery alieleza katika taarifa kwamba ‘mapungufu na kushindwa kwa May kumezuia kabisa serikali kusonga mbele katika wakati huu muhimu kwa nchi”.

Bado haijafahamika kama kura itamsaidia May kupata uungaji mkono anaouhitaji sana kwenye makubaliano ya Brexit ambayo anafanya majadiliano nao.

Uingereza inatarajia kujitoa kutoka Umoja wa Ulaya Machi 29 mwakani, ikiwa ni matokeo ya kura ya maoni ya mwaka 2016. Pande hizo mbili zilifanya kazi misingi ya kuachana baada ya mashauriano marefu, lakini lazima yaidhinishwe na bunge la Uingereza. Mapema wiki hii, May aliakhirisha upigaji kura uliopangwa ambao ulionekana ungefeli.

Theresa May, Waziri Mkuu wa uingereza
Theresa May, Waziri Mkuu wa uingereza

May amekuwa akijaribu mara kwa mara kuokoa mkataba kupitia mazungumzo na viongozi wa ulaya. Lakini maafisa wa EU wamekuwa thabiti kuhusu kutokuwa na hamu ya kufanya tena mashauriano kwa misingi hiyo.

Rais wa baraza la Umoja wa ulaya, Donald Tusk alisema baada ya kile alichokiita “mazungumzo marefu na ya wazi” na May siku ya Jumanne kwamba ni Dhahiri wanachama wengine wa EU wanataka kusaidia kutatua hali hii lakini “swali linakuja kwa njia ipi?”

Tusk ameitisha mkutano na viongozi wa EU hivi leo Alhamisi kuzungumzia Brexit ikiwemo uwezekano kwamba Machi 29 itafika na hakuna makubaliano yaliopo.

XS
SM
MD
LG