Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 11:04

Theresa May ashindwa vibaya katika kura ya Brexit


Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akihutubia bunge
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akihutubia bunge

Waziri Mkuu wa Uingereza ameshindwa vibaya katika kura ya kujitoa katika Umoja wa Ulaya - maarufu kama Brexit - katika bunge la Uingereza baada ya wabunge kupinga mswaada wake kwa kura 432 kwa 202.

Mara baada ya kipigo hicho, Bibi May alisema kutokana na wingi wa kura za kupinga mswaada huo serikali yake itaruhusu mswaada wa kutokuwa na imani kujadiliwa bungeni.

Wakati anarudi kukaa chini, kiongozi wa chama cha upinzani cha Leba Jeremy Corbyn, mara moja alithibitisha kuwa amewasilisha kura ya kutokuwa na imani na serikali ya May, mswaada ambao utajadiliwa Jumatano.

Bibi May alikuwa amewasilisha mbele ya bunge mpango mzima wa jinsi Uingereza itakavyojitoa katika Umoja wa Ulaya swala ambalo liliidhihishwa katika kura ya maoni mwaka 2016.

XS
SM
MD
LG