Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 10:54

Uingereza : May akabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye


Waziri Mkuu Theresa May
Waziri Mkuu Theresa May

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May anakabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye Jumatano baada ya wabunge kupinga kwa kauli moja mpango wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.

Wabunge kwa sauti moja walipiga kura dhidi ya mpango wa May ambao ulikuwa unataka kumaliza ndoa kati ya Uingereza na Umoja wa Ulaya.

Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani cha Labour, Jeremy Corbyn ametangaza kuwa amepeleka muswada wa kutokuwa na imani na serikali hiyo mara tu baada ya matokeo ya kura ya Brexit kutolewa Jumanne.

Iwapo May atashindwa, Uingereza italazimika kufanya uchaguzi mkuu.

Lakini wachambuzi wa kisiasa wanasema wanategemea kuwa May ataweza kubakia madarakani kwa kura hiyo kutofanikiwa kumuondosha.

Nacho chama cha walio wachache cha Ireland Kaskazini ambacho May anakitegemea ili serikali yake ya wachache iendelee kuwa madarakani kimesema kitaendelea kuiunga mkono serikali yake.

XS
SM
MD
LG