Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 06:21

May kujiuzulu mapema ikiwa wabunge watakubaliana na mpango aliojadiliana na Umoja wa Ulaya


Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May

“Nafahamu kwamba kuwa matamanio ya njia mpya na uongozi mpya katika hatua ya pili ya mazungumzo ya Brexit na sitaingilia hilo"-May

Siku zijazo za Brexit hazijulikani hata zaidi kwa sasa kuliko siku za awali baada ya Bunge la Uingereza Jumatano kukataa maombi 16 tofauti kwa serikali iliyokataa mara mbili maombi ya Uingereza kujitoa umoja wa Ulaya.

Bunge la Uingereza lilichukua mpango wa Uingereza kujitoa umoja wa Ulaya -Brexit kutoka kwa waziri mkuu Theresa May, ambaye mpaka sasa ameshindwa kupata makubaliano.

Wabunge walianza majadiliano Jumatano kukiwa na mipango tofauti 16. Wasuluhishi wamepunguzwa kufikia 8 waliokuwa wameletwa kupiga kura. Yote yalikataliwa.

Kati ya masuala mbadala ambayo wabunge walikataa jumatano ni moja ya ambalo lingeacha Uingereza na ushuru wa forodha na lile la kuweka swali la kuondoka Umoja wa Ulaya kwa kura nyingine ya maoni.

Umoja wa Ulaya umeipa Uingereza mpaka Aprili 12 kuwajulisha wanachama kile wanachopanga kufanya au itaacha Umoja wa Ulaya bila kuwa na mpango wa kutoka kitu ambacho kinaweza kupelekea ghasia za kiuchumi.

Waziri wa masuala ya Brexit Stephen Barclay, amesema kwamba ikiwa mapendekezo nane tofauti yameshindwa kufanikiwa ni ishara kwamba mpango wa May ulikuwa ni chaguo bora.

May amesema Jumatano kwamba atajiuzulu nafasi ya waziri mkuu mapema kuliko ilivyotarajiwa kama wabunge watakubaliana na mpango aliojadiliana na Umoja wa Ulaya.

“Nafahamu kwamba kuwa matamanio ya njia mpya na uongozi mpya katika hatua ya pili ya mazungumzo ya Brexit na sitaingilia hilo alisema Jumatano.

Imetayarishwa na Sunday Shomari.

XS
SM
MD
LG