Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 18:22

Brexit : Johnson asema 'tumepata makubaliano makubwa...'


Waziri Mkuu Boris Johnson
Waziri Mkuu Boris Johnson

Makubaliano ya Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya yamefikiwa na timu za ufundi zilizofanya majadiliano kabla ya mkutano wa viongozi wa Ulaya kuanza mjini Brussels.

Waziri Mkuu Boris Johnson alituma ujumbe wa tweet : " Tumepata makubaliano makubwa mapya ambayo yataendelea kuwa na mashiko."

Pande zote mbili zimekuwa zikifanyia kazi maandishi ya kisheria juu ya makubaliano hayo, lakini bado italazimu pande zote mbili za mabunge ya Uingereza na Umoja wa Ulaya kuyapitisha.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na viongozi wenzake 27 wa Umoja wa Ulaya wanakutana mjini Brussels Alhamisi katika kilelele cha mazungumzo wanayotegemea yatamaliza hasira na maudhi juu ya mvutano ulioendelea kwa miaka 3 wa Uingereza kujitoa katika umoja huo.

Hata kabla ya alfajiri, Johnson tayari alitakiwa akabiliane na vipingamizi vikubwa wakati washirika wa serikali ya Ireland ya Kaskazini wenzake waliposema hawataunga mkono pendekezo lake la kufikia muwafaka. Waziri Mkuu anahitaji msaada utakaoweza kupatikana ilikuweza kusukuma mbele makubaliano yoyote kuweza kupitishwa katika bunge lililogawanyika.

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP mkutano huo uliongeza wasiwasi mkubwa ambao Alhamisi asubuhi, wakati nyaraka za masuala ambayo yalikuwa hayajapatiwa ufumbuzi juu ya kujitoa Uingereza yakibakia hayaeleweki.

Kamati ya ufundi inayojadili mara nyingine ilikutana usiku Jumatano kurekebisha sheria za kodi ya forodha na mauzo ambazo zitaweza kudhibiti bidhaa katika biashara kati ya Ireland Kaskazini na Ireland, ambapo Uingereza na Umoja wa Ulaya unaunganishwa na mpaka pekee.

Walikuwa wamepangiwa kuendelea na mazungumzo mpaka wakati kilelele cha mkutano huo utakapofunguliwa mchana. Iwapo makubaliano yatafikiwa wakati wa mkutano huo wa siku mbili, Johnson anatarajia kuwasilisha katika Bunge la Uingereza makubaliano hayo katika Bunge la Uingereza katika kikao maalum Jumamosi

Umoja wa Ulaya umesema, mazungumzo juu ya BREXIT yanaendelea hivi sasa. Msemaji wa Umoja huo Mina Andreeva akieleza hali ya mazungumzo hayo amesema Raisi wa Halmashauri kuu ya Ulaya Jean-Claude Juncker anaendelea na mazungumzo na Johnson kufikia makubaliano mapya.

XS
SM
MD
LG