Mabalozi na maafisa waandamizi kutoka nchi nyingine 27 wanachama wa EU walikutana Jumapili baada ya wabunge wa Uingereza kumlazimisha Johnson kumtumia rais wa Baraza la EU Donald Tusk ombi la dakika ya mwisho kuahirisha kujitoa huko.
“EU inaangalia fursa zote zilizowazi katika suala hili na imeanzisha mchakato wa kupitisha makubaliano ili uweze kuwasilishwa katika Bunge la EU Jumatatu,” amesema mwanadiplomasia wa EU kuliambia shirika la habari la AFP.
“Huenda EU ikaendelea na mkakati huu mpaka pale itakapokuwa bayana kile Uingereza inachotaka,” amesema kwa sharti jina lake lisitajwe.
Tusk atatumia “siku chache” akiwashawishi viongozi wa nchi wanachama, na wanadiplomasia wamesema hii itamaanisha kuwa Bunge la Uingereza ni lazima lipige kura ya Brexit tena kabla ya kusikiliza uamuzi wao wa kujitoa ifikapo Octoba 31.
“Ulikuwa mkutano mfupi sana na wa kawaida wa mabalozi wa EU kuanzisha hatua zinazofuata za EU kupitisha mkataba huo,” mshiriki wa EU katika mazungumzo hayo Michel Barnier amewaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo ya Jumapili.
Wanadiplomasia wameiambia AFP mkutano wa mabalozi hao ulichukuwa dakika 15 na ulikuwa uaanglia kwa wepesi EU kupitisha suala hilo, japokuwa mshiriki mmoja amesema walikuwa wamepitia barua ya Johnson.
Alipoulizwa iwapo anafikiri kuwa viongozi wa EU wataruhusu kuchelewesha kufanyika maamuzi hayo, Barnier amesema : “Rais Tusk atatafuta ushauri siku chache zijazo.”