Wakati huo huo serikali ya Tanzania imekiri kuwepo mgogoro kati ya uwanja wa ndege wa Kimataifa wa KIA na wananchi. Katika repoti hii mwandishi wa VOA anakuletea taswira kamili ya mvutano huo na namna serikali inavyotoa ufafanuzi juu ya hatua madhubuti inazochukua kufikia suluhu. Lakini bado wanaharakati wa haki za kiraia wanaeleza vikwazo ambavyo wananchi wamejikuta matatani. Endelea kusikiliza...
Tanzania: Serikali yakiri kuwepo mgogoro kati ya uwanja wa ndege na wananchi
Wananchi katika maeneo ya hifadhi za taifa wapaza sauti zao kueleza umma kwamba eneo ambalo wanaishi wamelirithi kutoka kwa mababu zao. Watetezi wa haki za kiraia wanaeleza kuwa kwa kuibuka migogoro hii ni ishara kuwa kuna haja ya serikali kutafuta ufumbuzi wa mvutano huu uliopo sehemu mbalimbali.