Kaunda aliiongoza Zambia tangu mwaka 1994 wakati taifa hilo la kusini mwa Afrika lilipojipatia uhuru, hadi mwaka 1991. Ni miongoni mwa mashujaa wachache walioshiriki kuikomboa Afrika ambaye bado yuko hai.
Msaidizi wake Rodrick Ngolo amesema katika taarifa kwamba Kaunda amekuwa hajisikii vizuri na amelazwa katika hospitali ya Maina Soko mjini Lusaka.
Taarifa ya Ngolo inasema “ mheshimiwa Kaunda anaomba wa Zambia wote na jumuia ya kimataifa kumuombea wakati timu ya madaktari inafanya kila kitu kuhakikisha anapona.”
Chanzo cha Habari : Reuters