Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:11

WTO yaeleza kuongezeka pingamizi katika upatikanaji wa vifaa vya COVID-19


Ngozi Okonjo-Iweala
Ngozi Okonjo-Iweala

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Biashara (WTO) amesema Jumatatu pingamizi za kibiashara zinazohusiana na upatikanaji wa vifaa vya afya vinavyotumiwa dhidi ya COVID-19 zimeongezeka.

Pia amezisihi nchi wanachama kuondoa pingamizi hizo, wakati kunafanyika juhudi za kufikia makubaliano ya ugavi wa chanjo za COVID-19.

Ngozi Okonjo Iweala ameuambia mkutano wa Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao kwamba “hali hiyo inaelekea kwenye njia mbaya’’, akimaanisha pingamizi kwenye bidhaa za biashara zinazohusiana na janga la Corona.

Ameongeza kuwa “ kuna haja ya kuondoa vizuizi hivyo ili tupige hatua kwa kupata kwa haraka bidhaa za matibabu na chanjo.”

Iweala amesema pingamizi za biashara zilikua kwenye kiwango cha 109 wakati janga la Corona lilipojitokeza mapema mwaka 2020, na baadaye kiwango hicho kilishuka hadi 51, lakini tangu wakati huo kiliongezeka tena hadi 53.

Wakati huo huo ametoa wito kwa nchi wanachama wa WTO kufikia makubaliano kuhusu kuboresha upatikanaji wa chanjo za COVID-19 ikifapo mwezi Julai.

Chanzo cha Habari : Reuters

XS
SM
MD
LG