Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:27

Matumaini ya Ngozi Okonjo Iweala kuongoza WTO yaingia dosari


Dr Ngozi Okonjo-Iweala - Raia wa Nigeria
Dr Ngozi Okonjo-Iweala - Raia wa Nigeria

Marekani imeambia mkutano wa shirika la kimataifa la biashara(WTO) kwamba haimuungi mkono raia wa Nigeria Ngozi Okonjo Iweala kuongoza shirika hilo, licha ya mwanamama huyo kupata uungwaji mkono kutoka mataifa yaliyo nje ya bara la Afrika, vyanzo viwili vililiambia shirika la habari la Reuters.

Msimamo huo wa marekani unaweza kuidhoofisha taasisi hiyo ya biashara duniani ambayo inaendelea na mchakato wa kumpata kiongozi atakaechukua nafasi ya mkurungezi wa WTO raia wa Brazil Roberto Azevedo, ambae alijiuzulu mwezi Agosti.

Kundi kubwa la mabalozi wa WTO walipendekeza Okonjo Iweala awe mkurungezi wa shirika hilo, lakini uamuzi huo unahitaji makubaliano kati ya nchi 164 wanachama wa WTO, ikimaanisha kwamba nchi yoyote inaweza kuzuia uteuzi wa Okonjo.

Imetayarishwa na Patrick Nduwimana, VOA, Washington DC.

XS
SM
MD
LG