Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 17:01

Ngozi Okonjo Iweala mwanamke wa kwanza Mwafrika kuiongoza WTO


Ngozi Okonjo-Iweala mwanamke wa kwanza mwafrika kushikilia nafasi ya juu katika WTO
Ngozi Okonjo-Iweala mwanamke wa kwanza mwafrika kushikilia nafasi ya juu katika WTO

Okonjo Iweala mwenye miaka 66 atahitaji kushawishi mazungumzo ya biashara ya kimataifa kukiwa na mzozo unaoendelea wa Marekani na China, kujibu shinikizo la mageuzi ya sheria za biashara, na kinga ya kukabiliana na ongezeko la janga la Corona

Mkurugenzi mpya wa shirika la biashara duniani-WTO mwenye asili ya Nigeria, Ngozi Okonjo Iweala ameonya dhidi ya utaifa katika chanjo ya COVID-19 ambao kwa mtazamo wake utazorotesha maendeleo katika kutokomeza janga hilo na inaweza pia kukwamisha ukuaji wa uchumi kwa nchi zote, tajiri na maskini.

Katika mohojiano na shirika la habari la Reuters, Iweala amesema kipaumbele chake cha juu ni kuhakikisha WTO inaongeza juhudi kwa kukabiliana na janga la COVID-19 akisema nchi wanachama zinapaswa kuharakisha mchakato wa kuondoa vizuizi vya usafirishaji wa bidhaa zinazozorotesha biashara katika ugawaji wa dawa na vifaa vinavyohitajika.

Waziri huyo wa zamani wa fedha wa Nigeria na afisa mwandamizi wa zamani wa Benki ya Dunia aliteuliwa Jumatatu kwa kukubaliwa na nchi zote wanachama kuiongoza WTO na ataanza kazi yake hiyo mpya Machi mosi.

Kiongozi mpya wa WTO, Ngozi Okonjo-Iweala, Feb. 15, 2021.
Kiongozi mpya wa WTO, Ngozi Okonjo-Iweala, Feb. 15, 2021.

“WTO inaweza kuchangia sana kwa kudhibiti janga hilo” Okonjo Iweala amesema. Ameongeza kuwa hakuna alie salama hadi kila mmoja awe salama na kwamba utaifa wa chanjo hautokua na manufaa yoyote kwa sababu ya aina mpya ya virusi vya corona ambavyo vimetokea.

Okonjo Iweala amesema utafiti umeonyesha kwamba uchumi wa dunia utapoteza dola trillioni 9 katika mapato yanayotarajiwa ikiwa nchi maskini zitashindwa kuchanja raia wake kwa haraka na nchi tajiri zitajitwisha nusu ya athari hizo.

XS
SM
MD
LG