Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Januari 24, 2025 Local time: 06:29

EAC yamuidhinisha Amina Mohamed wa Kenya kwa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa WTO


Jumuia ya Afrika Mashariki Jumapili ilimuidhinisha  waziri wa Spoti na utamaduni wa Kenya, Amina Mohamed, kama mgombea wao katika uongozi wa Shirika la Biashara Duniani (WTO).

Hatua hiyo inaongeza uwezekano wa kupata mwanamke wa kwanza katika historia kuliongoza shirika hilo.

Tangazo hilo lilitolewa siku mbili tu kabla ya WTO kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea wawili watakaowania nafasi ya uongozi katika shirika hilo.

Tangazo hilo limetolewa na mwenyekiti wa mawaziri wa EAC Vincent Biruta kutoka Rwanda, ambaye alisema:

"Ningetaka kuwafahamisha kuwa balozi Amina C. Mohamed ameidhinishwa kuwa mgombea wa jumuia ya Afrika mashariki kuchukua nafasi ya mkurugunzi mkuu wa WTO kufuatia ombi kutoka kwa mwenyekiti wa EAC rais Paul Kagame la kimuidhinisha."

WTO lenye makao yake makuu mjini Geneva Uswizi liko katika mchakato wa kujaza nafasi ya Roberto Azevedo kutoka Brazil ambaye ametangaza kuondoka kwenye wadhifa huo mwaka mmoja kabla ya muda wake kumalizika.

Atakae mridhi anatarajiwa kuwa na uwezo wa kuongoza shirika hilo wakati ulimwengu ukishuhudia misukasuko ya kiuchumi, janga la corona na taharuki ya kibiashara hasa kati ya Marekani na China.

Amina Mohamed anadaiwa kuwa na uzoefu mkubwa kwenye WTO kutokana na kuwa aliwahi kuwa balozi wa Kenya kwenye shirika hilo na pia mwanamke wa kwanza kuwa mwenyekiti wa baraza kuu mwaka 2005.

Mohamed alikuwa miongoni mwa wagombea 6 walioteuliwa kuwania uongozi wa WTO wengine wakiwa ni Ngozi Iweala kutoka Nigeria, Yoo Myung , Korea kusini, Mohammad Maziad Al Tuwaijri kutoka Saudi Arabia na Liam Fox kutoka Uingereza miongoni mwa wengine.

Kwa kawaida kiongozi wa WTO hudhinishwa kupitia makubaliano ya mataifa wanachama 164 wa shirika hilo ambapo mshindi anatarajiwa kutangzwa kufikia Decemba mwaka huu.

Wakati huu kunaonekana kuwa na makubaliano kwamba ni wakati wa Afrika kutoa kiongozi wake . Iwapo Mohamed au Iweala watapata nafasi hiyo, basi itakuwa mara ya kwanza kwa mwanamke kuongoza WTO na pia mara ya kwanza kwa kiongozi wake kutoka barani Afrika

. WTO lilibuniwa mwaka 1995 kwa nia ya kusimamia biashara a kimatifa pamoja na kutatua migogoro kati ya mataifa.

-Imetayarishwa na Harrison Kamau, VOA, Washington DC

XS
SM
MD
LG