Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 07:10

Kiongozi wa Myanmar Suu Kyi afikishwa mahakamani


FILE - Waandamanaji wakishinikiza jeshi la Myanmar kumuachia huru Aung San Suu Kyi, in Yangon, Myanmar, Feb. 6, 2021.
FILE - Waandamanaji wakishinikiza jeshi la Myanmar kumuachia huru Aung San Suu Kyi, in Yangon, Myanmar, Feb. 6, 2021.

Kiongozi wa Myanmar aliyeondolewa madarakani Aung San Suu Kyi Jumatatu amefikishwa mahakamani katika mji mkuu wa nchi hiyo akikabiliwa na mashtaka kadhaa yanayohusiana na ufisadi yaliyowasilishwa dhidi yake na utawala wa kijeshi ambao ulichukua madaraka zaidi ya miezi minne iliyopita.

Suu Kyi mwenye umri wa miaka 75 anakabiliwa na mashtaka ya kumiliki kinyume cha sheria vifaa vya mawasiliano visivyokua na kibali na kukiuka masharti ya kupambana na janga la COVID-19, wakati alipofanya kampeni ya uchaguzi wa bunge mwaka 2020.

Mawakili wake waliwaambia waandishi wa habari kwamba wanatarajia kesi hiyo itaendelea kusikilizwa hadi mwishoni mwa mwezi Julai.

Mshindi huyo wa tuzo ya amani ya Nobel anazuiliwa tangu tarehe 1 Februari, wakati serekali yake ya kiraia ilipoondolewa madarakani miezi mitatu baada ya chama chake National League for Democracy kupata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi wa bunge.

Viongozi wa kijeshi wanamshtumu pia Suu Kyi kwa makosa kadhaa ikiwemo kukubali malipo ya pesa haramu taslimu dola laki 6 pamoja na kilo 11 za dhahabu.

Phil Robertson, naibu mkurugenzi wa shirika la haki za binadamu katika Human Rights Watch kanda ya Asia, leo amesema katika taarifa kwamba mashtaka yote hayo yanatakiwa kufutwa, na hivyo Suu Kyi aachiliwe huru mara moja bila masharti yoyote.

Chanzo cha Habari : VOA News

XS
SM
MD
LG