Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 14:55

Wafanyakazi Myanmar waandamana kupinga utawala wa kijeshi


Waandamanaji wakiwakimbia polisi huku wakiendelea kupinga mapinduzi ya kijeshi mjini Yangon, Myanmar, Machi 8, 2021. REUTERS/Stringer
Waandamanaji wakiwakimbia polisi huku wakiendelea kupinga mapinduzi ya kijeshi mjini Yangon, Myanmar, Machi 8, 2021. REUTERS/Stringer

Muungano wa vyama 9 vya wafanyakazi nchini Myanmar mapema Jumatatu umejiunga kwenye maandamano yanayo endelea kushuhudiwa nchini humo ili kushinikiza kuondoka kwa utawala wa kijeshi uliofanya mapinduzi ya serikali.

Kupitia kwenye taarifa ya pamoja, muungano wa wafanyakazi umesema kuendelea na shughuli za kawaida za kiuchumi kunawanufaisha wanajeshi hao ambao wameendelea kukandamiza watu wa Myanmar.

Maandamano kutoka kwa wafanyakazi wa serikali wakiwemo wale wanaofanya kwenye treni yamekuwa yakiendelea nchini humo kwa muda wa wiki kadhaa sasa.

Shirika la habari la Reuters limesema kuwa waandamanji kwenye mji mkuu wa Yangon wameonekana wakibeba vibendera vidogo kuadhimisha siku ya wanawake duniani huku huduma muhimu kama maduka na benki yamefungwa.

Afisa mmoja kutoka chama cha National League for Democracy cha kiongozi wa kiraiya aliyezuiliwa Aung San Suu Kyi ameithibitishia VOA kwamba mmoja wa maafisa wa chama hicho amefariki wakati akiwa kizuizini.

Kundi linalotetea haki za wafungwa wa kisiasa limesema Jumamosi kuwa zaidi ya watu 1,700 wamezuiliwa tangu mapinduzi yakijeshi yalipofanyika mwezi uliyopita.

XS
SM
MD
LG