Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Septemba 08, 2024 Local time: 03:03

Myanmar : Vyombo vya usalama vyarusha risasi kuwatawanya waandamanaji


Myanmar, Yangon, People shout slogans during a protest against the military coup
Wananchi wakipaza sauti kupinga mapinduzi ya kijeshi wakati wa maandamano mjini Yangon, Myanmar Februari 26, 2021.REUTERS/Stringer
Myanmar, Yangon, People shout slogans during a protest against the military coup Wananchi wakipaza sauti kupinga mapinduzi ya kijeshi wakati wa maandamano mjini Yangon, Myanmar Februari 26, 2021.REUTERS/Stringer

Polisi na vikosi vya usalama katika mji mkubwa zaidi nchini Myanmar walifyatua risasi za kuwaonya waandamanaji Ijumaa.

Risasi hizo zilirushwa wakati vyombo hivyo vya usalama vilipokuwa vikisogea kuvunja kundi la waandamanaji wapatao elfu moja.

Waandamanaji hao walikuwa wamekusanyika katika jumba maarufu la maduka katika kitongoji cha Tamwe cha Yangon usiku kupinga afisa aliyeteuliwa na jeshi.

Waandamanaji walikuwa wakishikilia mabango na wakipiga kelele wakilaani mapinduzi ya Februari mosi, licha ya kuongezeka kwa uwepo wa vikosi vya usalama na lori la maji ya kuwasha lililokuwa katika eneo hilo.

Kulingana na vyombo vya habari vya serikali na mashuhuda kitengo cha karibu polisi 50 wa kutuliza ghasia walichukua hatua dhidi ya waandamanaji na kumkamata mwandamanaji mmoja.

Shirika la habari la Reuters linaripoti kuwa mwandishi wa habari wa Kijapani alikamatwa kwenye maandamano huko Yangon Ijumaa. Kama ikithibitishwa, ukamataji huo utakuwa ni wa kwanza kwa mwandishi wa habari wa kigeni tangu mapinduzi.

XS
SM
MD
LG